YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumatano, 16 Machi 2016

Ratiba ya Ligi Kuu yaongezwa viraka

MECHI mbili za viporo za Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara za Azam na Yanga zilizopangwa kufanyika mapema wiki ijayo, zimeahirishwa kupisha ratiba ya timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ katika mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2017.
Mechi hizo ni kati ya Mtibwa Sugar na Azam FC iliyokuwa ichezwe Machi 22 kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro na Yanga dhidi ya Mwadui FC, Machi 23, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), Baraka Kizuguto alisema Taifa Stars itakuwa na mchezo wa kufuzu Afcon dhidi ya Chad mjini ND’jamena Machi 25 na zitarudiana Machi 28 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
“Kutokana na ratiba ilivyo baada ya mechi za mwishoni mwa wiki za hii za michuano ya klabu Afrika, wachezaji wa Taifa Stars wanatarajiwa kukusanyika Jumapili kabla ya safari Jumanne kuelekea Chad,” alisema Kizuguto.
Yanga watarudiana na APR ya Rwanda Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Yanga walishinda mabao 2-1.
Nayo Azam FC itarudiana na Bidvest Wits ya Afrika Kusini Jumapili, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam baada ya kushinda 3-0 huko Johannesburg. Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 54 kwa michezo 23 imekuwa ikilalamika kwamba Yanga na Azam zina mechi nyingi za viporo hivyo kutaka zimalize kwanza mechi zake.

Vinara hao wa ligi wameizidi Azam kwa mechi tatu na Yanga mechi mbili. Simba Jumamosi itacheza na Coastal Union ya Tanga. Akizungumzia suala hilo, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema leo atazungumzia masuala mbalimbali yakiwemo ya mabadiliko ya ratiba kwa mechi za viporo kwa baadhi ya timu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads