YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumatano, 16 Machi 2016

RC kusimamia Shilingi milioni 50 za kila kijiji

KAZI ya kusimamia Sh milioni 50 zilizopangwa kutolewa kwa kila kijiji kwa ajili ya kukabili umasikini wamepewa wakuu wa mikoa. Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu alisema jana kwamba Serikali imejiandaa kutimiza ahadi ya kutoa fedha hizo na utekelezaji wake, utaanza katika bejeti ijayo ya mwaka 2016/2017.
Akizungumza baada ya wakuu hao wa mikoa kutia saini kiapo cha utii, Ikulu Dar es Salaam , Samia alisema fedha hizo lengo lake ni kupunguza umasikini kuanzia ngazi ya chini. “Najua kuna taasisi mbalimbali zimekuwa zikiwafikia na kuwasaidia wananchi katika hili ukiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) lakini bado kuna kazi kubwa ya kuwafikia wananchi masikini,” alisema Mama Suluhu.
Alisema fedha hizo zimeanza kuingizwa kwenye bajeti hiyo na zinategemewa kusambazwa katika vijiji vyote mwanzoni mwa utekelezaji wa bajeti hiyo. “Napenda niwafikishie maagizo ya Rais John Magufuli kwenu kuwa fedha hizi zinakuja kwenu zisimamieni ili zifanye kazi iliyokusudiwa,” alisisitiza.
Awali kabla ya viongozi hao kutia saini hati hiyo ya kiapo cha utii, Kamishna Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili, Jaji Salome Kaganda, alisema hati hiyo ya kiapo cha maadili ni lazima kila kiongozi aisaini kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Aliwataka wakuu hao wa mikoa ambao hawakubaliani na kiapo hicho cha utii kuhakikisha kuwa hawasaini hati hiyo na hivyo sekretarieti hiyo itawasilisha majina yao kwa Rais Magufuli ikiwa ni ishara kwamba wameukataa uteuzi wake.


Hata hivyo, wakuu hao wa mikoa kwa pamoja walisoma kwa sauti kiapo hicho ambacho kinawataka kuheshimu wadhifa wao, kuepuka rushwa, kutokutoa siri za ndani katika kazi zao, kuwahudumia wananchi, kupambana na ubadhirifu na ufisadi lakini pia kusimamia maendeleo pamoja na usalama wa mikoa yao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads