Utafiti wa karibuni zaidi umeonesha kwamba njia bora zaidi ya kuacha uraibu wa kuvuta sigara ni kuacha mara moja.
Utafiti ambao matokeo yake yamechapishwa katika jarida la kimatibabu la Annals of Internal Medicine unasema washiriki walioacha mara moja walikuwa na uwezekano mara 25% zaidi ya kutovuta sigara nusu mwaka baada ya kuachana na uraibu huo wakilinganishwa na walioacha uvutaji sigara taratibu taratibu.
Idara ya Afya ya Taifa Uingereza inasema njia bora zaidi ni kutenga siku fulani kuwa ya kuacha kuvuta sigara.
Weka ahadi, tenga siku na uhakikishe umefanya hivyo siku hiyo, idara hiyo inashauri.
Utafiti huo wa karibuni uliofadhiliwa na Wakfu wa Moyo wa Uingereza ulihusisha washiriki 700 wa kujitolea.
Waliwekwa kwenye makundi mawili, moja la kuacha kuvuta sigara mara moja na jingine la kuacha asteaste.
Baada ya miezi sita, ni 15.5% ya washiriki walioacha kuvuta sigara taratibu taratibu waliokuwa bado hawavuti sigara wakilinganishwa na 22% kwenye kundi la walioacha kuvuta sigara mara moja.
Kiongozi wa utafiti huo Dkt Nicola Lindson-Hawley, kutoka Chuo Kikuu cha Oxford alisema: "Tofauti inaonekana ni kama inatokana na kutatizika kwa watu katika kupunguza uvutaji sigara. Hili liliwapa jambo la ziada la kufanya, ambalo huenda liliwafanya kuacha kabisa mpango wao wa kuacha uvutaji sigara.”
Ingawa wengi wa washiriki walisema wangependelea sana kuacha uvutaji sigara, bado wale waliofanikiwa zaidi kuacha kabisa uvutaji sigara walikuwa wale walioacha Dkt Lindson-Hawley hata hivyo alisema ni heri kupunguza uvutaji sigara kuliko kutochukua hatua yoyote.
Washiriki wote walipewa ushauri pamoja na vitu vya kuwasaidia kukabiliana na makali ya kuacha uvutaji sigara.
Source: BBCSwahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni