Mwishoni mwa wiki jana, Guzman alikaririwa akisema kuwa, Chris aekuwa akivuta sigara karibu na mazingira alipo mtoto wao huyo, hivyo kumsbabishia mtoto ugonjwa wa pumu (asthma).
“Nilishaacha uvutaji wa sigara tangu kitambo,” aliandika hivyo. “Hakuna mtu yeyote anavuta sigara karibu na mwanangu… Ninajari na kumthamini mwanangu na siwezi kumuweka kwenye mazingira ambayo yatamdhuru.”
Brown aliongeza kuwa, madai ya mzazi mwenzake ilikuwa anataka apewe pesa ili aongeze kipato chake. Kulingana na ripoti ya jarida la TMZ, Guzman anahitaji pesa kiasi cha dola za Marekani 16,000 kila mwezi kwa ajili ya atuizi ya mtoto, ikiwa ni ongezeko kubwa kutoka kiasi cha dola za Marekani 2,500 anazopewa kwa sasa kulinagana na makubaliano.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni