Hebu vuta picha, ni saa nane za usiku
unakimbizana na muda kuwahi kurudi nyumbani baada ya kuchelewa kwenye
mihangaiko yako, ukiwa unakatiza mitaa ya karibu na ikulu, unakutana na
kitu kinachokufanya usiyaamini macho yako.
Unakutana uso kwa uso na mheshimiwa rais, akiwa anayumbayumba
kutokana na kuzidiwa na pombe, tena akiwa amevaa bukta ya kulalia tu,
yuko bize kusimamisha teksi eti zimpeleke kwenye mgahawa ambao uko wazi
akanunue msosi kwa sababu anasikia njaa kali. Utahisi upo ndotoni si
ndiyo?
Basi kwa taarifa yako tukio kama hilo limewahi kumkumba aliyekuwa
Rais wa Urusi, Boris Yeltsin. Wakati wa utawala wa Rais Bill Clinton wa
Marekani, mwaka 1995 alimualika Yeltsin, akiwa rais wa Urusi wakati huo
kwenda kumtembelea kwenye Ikulu ya White House jijini Washington.
Sifa kubwa ya Yeltsin, kabla hajawa rais, alipokuwa rais na mpaka
alipostaafu, ilikuwa ni kupiga mitungi mpaka anakuwa chakari. Basi baada
ya shughuli zote za kiofisi kukamilika ikulu, jamaa alianza kujimiminia
Vodka kwa uchu mpaka akawa tilalila. Kibaya alikuwa anakunywa bila
kugonga msosi.
Akapitiwa na usingizi lakini mishale ya saa nane za usiku,
alizinduka, pombe zikiwa bado kichwani na kukumbuka kwamba hakula usiku
huo zaidi ya kupiga maji. Kutokana na njaa iliyokuwa inamsumbua, akaona
isiwe tabu, akatoka akiwa amevaa bukta na kuwazidi ujanja walinzi wa
ikulu, akaingia mitaani na kuanza kupiga kelele kusimamisha teksi
impeleke kununua pizza.
Walinzi wa ikulu kuja kushtukia, rais tayari alishafika Mtaa wa
Pennsylvania huku akiendelea kufanya mambo ya kilevi, wakagundua kuwa
kumbe mtu huyo alikuwa rais wa Urusi, wakawa wanajiuliza imekuwaje
awapite bila kumtambua?
Harakaharaka wakaenda kumchukua na kumrudisha ndani huku mlinzi mmoja
akitumwa kwenda kumnunulia pizza kwani mwenyewe bado alikuwa
akilalamikia njaa.
Kutokana na itifaki za White House, tukio hilo lilifanywa kuwa siri
kubwa kuanzia siku linatokea mpaka miaka kumi baadaye, Rais Bill Clinton
ndiye aliyeamua kulisimulia alipoamua kuandika kitabu cha kumbukumbu za
maisha yake.
Kwa mara ya kwanza, Clinton alimsimulia mwandishi Taylor Branch
aliyeandika kitabu cha historia ya Clinton kilichopewa jina la The
Clinton Tapes: Wrestling History with the President. Rais Yeltsin
alifariki miaka miwili iliyopita baada ya kuugua.
Source:GlobalPublishers
Translate
Jumatano, 3 Februari 2016
Home
/
Habari Kali Za Siku
/
Vituko/Comedy
/
yc
/
Kuhusu Boris Yeltsin: Raisi 'Chapombe alietoroka ikulu usiku wa manane kwenda kusaka msosi
Kuhusu Boris Yeltsin: Raisi 'Chapombe alietoroka ikulu usiku wa manane kwenda kusaka msosi
About Young Concious
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
yc
Lebo:
Habari Kali Za Siku,
Vituko/Comedy,
yc
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni