Nahodha wa timu ya taifa ya Ghana Asamoah Gyan leo amethibitisha kujiunga na klabu ya Shanghai SIPG ya China kwa mkataba wa miaka miwili.
Nyota huyo aliyeisaidia timu yake ya
Ghana kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali ya kimataifa atakua
akilipwa dola 250,000 kwa wiki sawa na zaidi ya milioni 500.
Asamoah amesaini mkataba huo mbele ya kaka yake Baffour na meneja wake Samuel Anim Addo na atatambulishwa katika mechi ijayo ya ligi kuu ya China dhidi ya Guangzhou R&F.
Asamoah amejiunga na timu hiyo akitokea klabu ya Al Ain ya falme za kiarabu ambayo amedumu nayo kwa miaka minne, ameichezea mechi 83 na kuifungia mabao 95.
Source; MillardAyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni