| Nokia |
Chini ya mkataba wa kununua hisa zote,wamiliki wa hisa za
Alcatel-Lucent watamiliki asilimia 33.5 ya kampuni hiyo mpya huku
wamiliki wa hisa za Nokia wakichukua asilimia 66.5.
Kampuni zote
mbili zimesema kuwa wakurugenzi wake wamekubaliana ununuzi wa
Alcatel-Lucent na wanatarajia mpango huo kuafikiwa katika nusu ya kwanza
ya mwaka ujao.Muungano huo utabuni kifaa cha mawasiliano barani Ulaya kitakachogharimu yuro billioni 40.
Mkuu wa kampuni ya Nokia Rajeev Suri amesema kuwa kampuni hiyo ilio na teknologia chungu nzima itawasaidia kuongeza ujuzi katika kila sehemu watakayochagua kushindana.
''Ninaamini kwamba huu ni mpango kabambe uliofanyika wakati mzuri.''
Source: BBC

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni