Marekani imetangaza rasmi utaratibu mpya
ambao unaowalazimu abiria wanaosafiri kwa ndege kuingia nchini humo
wakitokea Afrika Magharibi, kushuka katika moja ya viwanja maalum vitano
ambavyo vimetengwa.
Utaratibu ambao Marekani imeuweka
unawalazimu wasafiri wote kutoka nchi za Liberia, Guinea na Sierra Leone
kuingia nchini humo kwa kupitia moja viwanja vya O’Hare Chicago, JFK,
Newark, Washington Dulles au Atlanta.
Marekani imeweka utaratibu huo ambapo
viwanja hivyo vina wataalamu na mashine maalum za kufanyia uchunguzi wa
virusi vya ugonjwa huo.
Leo kamati ya dharura ya shirika la afya
duniani WHO imefanya mkutano huku lengo kuu likiwa ni kutathmini juhudi
zilizofikiwa za kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.
Japo WHO imetangaza kutekeleza mpango wa
chanjo ya kinga ya Ebola katika ukanda wa Afrika Magharibi matumaini
bado ni madogo mpaka sasa ambapo zaidi ya watu 4,700 wameripotiwa
kufariki kwa ugonjwa huo.
Source:MillardAyo

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni