YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Alhamisi, 24 Aprili 2014

Tatoo yamzuia mtu kuingia Srilanka,Kisa Soma hapa zaidi

Cheki jinsi Tatoo hii ya Dini ilivyomsumbua mtalii huyu.

mtaliiUnaambiwa Mtalii mmoja raia wa Uingereza amekataliwa kuingia nchini Sri Lanka baada ya kupatikana akiwa na Tattoo ya dini ya Budhaa kwenye mkono wake.
Naomi Michelle Coleman alikamatwa na maafisa wakuu alipowasili katika uwanja wa ndege katika mji mkuu Colombo baada ya maafisa wakuu kuiona Tattoo hiyo kwenye mkono wake wa kulia.
Tafsiri ya dini hiyo kulingana na Budhaa mwenyewe inasemekana alikuwa mtu mwenye busara na hekima kubwa na pia mwanzilishi wa dini hiyo ambayo mafunzo yake mengi yalijenga msingi wa dini yenyewe.
Msemaji wa polisi amesema kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 37 alikamatwa kwa kosa la kuwachukiza watu wa dini ya Budhaa na pia kwa kuumiza hisia zao za kidini ambapo Hakimu aliamuru Bi.Coleman kurejeshwa nchini kwao.
Kwa sasa amezuiliwa katika kituo cha wahamiaji wanaosubiri kurejeshwa makwao na inasemekana Maafisa huchukua hatua kali dhidi ya watu wanaonekana kutusi dini ya Budhaa ambayo waumini wake wengi wanatoka kabila la Sinhalese lenye idadi kubwa ya watu nchini humo.
budhaaBi Coleman aliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bandaranaike siku ya Jumatatu kutoka nchini India ambapo maafisa baada ya kuiona Tattoo hiyo ya Budhaa akiwa amekaa kwenye mauwa walimkamata.
Kwenye kumbukumbu Mwezi Machi mtalii mwingine muingereza, alizuiwa kuingia katika uwanja huo baada ya maafisa kusema kuwa alijibu kijeuri alipohojiwa kuhusu Tattoo aliyokuwa amechorwa ambayo pia ilikuwa na Budhaa.
Source: MillardAyo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads