YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Ijumaa, 21 Machi 2014

Je Umeisikia hii mpya kutoka Saudi Arabia,Icheki hapa sasa!!?


Kuanzia sasa, mtoto yeyote atakaezaliwa Saudi Arabia haruhusiwi kupewa haya majina


Screen Shot 2014-03-21 at 5.23.39 AMWizara ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia imepiga marufuku majina hamsini ambayo yapo kinyume na tamaduni pamoja na dini ambapo kuanzia sasa, wazazi kutoka falme hiyo hawataruhusiwa tena kuwapa watoto wao.
Majina hayo ni kama Linda, Alice, Elaine au Binyamin (jina lenye maana Benjamin) ambapo jina la Benjamin (Binyamin) kwa dini ya kiislamu linaaminika kuwa jina la mtoto wa mtume Jacob, yaani Yacoub kwa dini.
Mengine katika orodha hiyo ambayo hayatoruhusiwa ni kwa sababu yanaaminika kuwa yenye kufuru, yasiyo ya kiarabu na yasio ya kiislamu au yenye kupingana na tamaduni na dini ya falme hiyo.
Sababu nyingine ni ya kigeni ama ya ughaibuni yakiwemo yenye maana ya ufalme au ukubwa, cheo flani kama Sumuw (mtukufu), Malek (mfalme) na Malika (Malkia).
Screen Shot 2014-03-21 at 5.23.23 AMMajina mengine hayapo katika jamii hizi hivyo hakuna sababu zilizotolewa juu yake, hii ni sehemu nyingine ya orodha yenyewe ambapo ni Malaak (angel), Abdul Aati, Abdul Naser, Abdul Musleh, Binyamin (Arabic for Benjamin) Naris, Yara, Sitav.
Mengine ni Loland, Tilaj, Barrah, Abdul Nabi, Abdul Rasool, Sumuw (highness), Al Mamlaka (the kingdom), Malika (queen), Mamlaka (kingdom), Tabarak (blessed), Nardeen, Sandy, Rama (Hindu god), Maline, Elaine, Inar, Maliktina
Maya.


Source: MillardAyo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads