Muoenekano wa ujenzi wa mradi wa daraja la Kigamboni katika awamu ya kwanza ukiwa umekamilika kwa asilimia 47, katika mradi huo. Ujenzi huo utagharimu jumla ya Sh. Bilioni 214, kati ya fedha hizo asilimia 60 zimetolewa na Shirika la Hifadhi ya Mfuko wa Jamii (NSSF). Picha hii imepigwa wakati Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (hayupo pichani) alipofanya ziara ya siku moja ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi ya Miundombinu hiyo ya jijini Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na ujenzi wa daraji hili.
Picha ya Daraja hilo kama ilivyopigwa kutoka juu inavyoonekana.
Sehemu ya Daraja la muda litakalotumika kwa ajili ya kupitishia vifaa vya ujezi wa Daraja la Kigamboni likiwa linaendelea kujengwa kwa ajili ya kuanza shughuli rasmi za ujenzi wa Daraja la Kigamboni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni