LIST YA BRAND ZA T-SHIRTS AMBAZO ZINAUZA SANA SOKONI..!!
VANESSA MDEE-#Money14
Muite
Vanessa Mdee aka VeeMoney ,ni mwanamuziki pia ni mtangazaji…Mwanadada
huyu ndiye mmiliki wa logo ya #Money14 ,ni moja kati ya idea yakipekee
katika upande mzima wa design ya tshirt zake,imekaa kimtindo wa tshirt
na wakati huo huo kama jezi.watu wengi hata baadhi ya wasanii wenzake
wameonekana kuvutiwa na vazi la Vanessa.
DIAMOND PLATNUMZ-WASAFI CLASSIC BABY(WCB)
Diamond
Platnumz aka raisi wa wasafi, ndio mmiliki wa brand ya Wasafi Classic
Baby(WCB),akiwa kama mwanamuziki ambaye ni maarufu sana EastAfrica na
nje ya Africa,baada ya kampuni yake ya wasafi ku-make headlines
nchini,bila kuchelewa akaingiza mzigo huu wa nguo za wasafi classic
baby,zipo kwa kila design ya maneno hayo ya wasafi,ni moja kati ya logo
nzuri sana kuivaa,hapo unakuta kofia,Tshirt hadi viatu vya Wasafi
utavipata
OMMY DIMPOZ –PKP
Ommy
dimpoz ndio mmiliki wa kampuni yake binafsi inayoitwa PozkwaPoz, ambayo
ndio imepelekea brand logo ya PkP,so far ameweza ku-release kofia za
PkP na ahadi yake ni kwamba,tusubiri mengi kutoka kwake kwa upande mzima
wa mavazi,sababu huo ni mwanzo tu.
IZZO BIZNESS –T UMOGHELE25
Izzo
Bizness msanii maarufu wa mtindo wa crank hapa bongo, anayepeperusha
vizuri bendera ya huko alipotokea jijini mbeya, Izzo naye anamiliki
design logo ya TUMOGHELE 25, huku namba 25 ikiwa ni namba ya muhimu sana
kwake, tarehe 25 ndiyo siku alipopigiwa simu na master J kumuita aanze
kurekodi, kuanza kazi rasmi, na tarehe ya 25 ni siku yake ya kuzaliwa.
Ukiangali ni moja kati ya design kali sana na yakipekee ya tshirt,
tshirt hizi zilitoka na kuambatana na video iliyopewa jina la Tumoghele.
#TeamMatagi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni