Ratiba
ya hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani ulaya imepangwa hii leo
huko Nyon nchini Uswissi yalipo makao makuu ya shirikisho la soka barani
ulaya .
Ratiba
hiyo inaonyesha kuwa Mabingwa watetezi Bayern Munich watacheza na
Arsenal , timu iliyofika fainali msimu uliopita ya Borrusia Dortmund
itakipiga dhidi ya Zenith St Petersburg toka Urusi .
Michezo
mingine itazikutanisha Chelsea ya England na Galatasaray katika mchezo
ambao utawakutanisha Kocha Jose Mourinho na wachezaji wake wa zamani
Wesley Sneijder na Didier Drogba . Manchester United watacheza na
Olympiakos ya Ugiriki huku Real Madrid wakicheza na Schalke 04.
Mabingwa
zamani Fc Barcelona watacheza na Manchester City , Ac Milan watacheza
na Atletico Madrid huku Paris St Germain wakicheza na Bayer Leverkusen.
Michezo hiyo itapigwa kuanzia tarehe 18 , 19 , 25 na 26 mwezi Februari huku marudiano yakichezwa mwezi machi tarehe 12 , 13 , 18 na 19.
Arsenal vs Bayern Munich
Ac Milan vs Atletico Madrid
Galatsaray vs Chelsea
Manchester City vs Fc Barcelona
Bayer Leverkusen vs Paris St Germain
Schalke 04 vs Real Madrid
Olympiakos vs Manchester United.
Zenith St Petersburg vs Borrusia Dortmund.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni