
Tamasha
la Xxl Afta xkul Bash ndio sehemu ambayo nilimuona huyu jamaa baada ya
kujitokeza kwenye mashindano ya kumtafuta Mtu anaefanana na Star.
Nikaona si mbaya tukafahamu hata kwa uchache historia yake na anamjua vipi Marehemu Ngwea.

‘Mi
naitwa Mohamed au Junior weezy, junior weezy kwa sababu imekua Talk of
Town gumzo Town kila mtu Ngwea Ngwea,mi Ngwea namfaham kama artist so
nimeonana nae mara ya mwisho nikiwa mdogo lakini Jay Moe alimwambia
Ngwea unafanana sana na jamaa pale ndo ilikua mara yangu ya kwanza naya
mwisho kuonana na Ngwea’.

‘Yeah
ilikua mwaka 2003 baada ya Jay Moe kumwambia unafanana sana na dogo
alisema ndio kweli nafanana nae lakini mtu aliekuja kunifahamisha zaidi
ni Dully,Dully alisema unafanana sana na Ngwea na mpaka leo huwa
ananiita Ngwea.watu walinishawishi kulingana na hii sura nliyonayo watu
wamenishawishi taratibu naanza kuingia kwenye game bado sijafanya track
nipo njiani,nakutana na vituko vingi wengine wananikimbia wanasema
nimefufuka na vitu vingine vya ajabu nakutana navyo mtaani muda mwingine
nasisimka nahisi kama Mangwea yuko ndani ya mwili wangu,naweza kuimba
baadhi ya ngoma za Ngwea kama tupo juu..na baadhi ya ngoma zingne.
Source: MILLARDAYO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni