Inaitwa Fastjet ambayo ndiyo kampuni ya ndege pekee ya bei nafuu Africa inayotoza nauli ya bei nafuu na unasafiri kwa uhakika ambapo Ijumaa hii November 29 2013 wanafikisha mwaka mmoja na sasa wakiwa wanasafirisha abiria kwenye mikoa ya Dar Es Salaam kwenda Mbeya, Kilimanjaro, Mwanza na Zanzibar.
Sasa basi, wakiwa wanasherehekea huu mwaka mmoja… Fastjet wanatoa maelfu ya tiketi kwa bei ya chini kabisa ya shilingi 32,000 kwa safari za ndani ya nchi, kwa ufupi ni kwamba una safiri popote wanapofika Fasjet nchini kwa shilingi 32,000 na unatakiwa kusafiri kati ya tarehe 6 Januari na 29 March 2014.
Baadhi ya watu wa nguvu ambao ni sehemu ya waliowahi kuenjoy kusafiri na Fastjet kwenda Johannesburg.
Ukitembelea ofisi za Fastjet kwa ajili ya kununua tiketi Ijumaa tarehe 29 utakutana na mengi mazuri manake wanatoa pia zawadi za keki na vitu mbalimbali kutoka Fastjet kwa ajili ya kusheherekea siku ya kuzaliwa kwao hapa Tanzania ambapo Ofisi za Fastjet Dar Es Salaam zipo Nyerere Road, Samora Avenue na Double Tree, Arusha zipo Blue Plaza na Mwanza zipo Kenyatta Road.
Fastjet pia wamenzindua safari za kwenda Johannesburg kutokea Dar zikifanyika amara tatu kwa wiki yani Jumatatu, Jumatano na Ijumaa na ticket zinauzwa kwa bei nafuu ya shilingi 160,000 hivyo tafuta Fastjet kwenye google utapata mambo meeeengi, tembelea fastjet.com, wapo facebook, twitter (@fastjet) na instagram (@fastjetofficial)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni