YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Ijumaa, 2 Agosti 2013

Uruguay yakaribia kuwa nchi ya kwanza kuruhusu kulima, kuuza, kutumia bangi

Nchi ya Uruguay huenda ikaweka rekodi kuwa
nchi ya kwanza Duniani kuruhusu na
kuhalalisha rasmi kulima, kusambaza na kuuza
(biashara) bangi.
Rais wa nchi hiyo, Jose Mujica ameunga
mkono hatua ya kuwasilishwa muswada
Bungeni ambapo wajumbe wakiupitisha,
watakuwa wamefanikisha lengo lake alilolisema
ni njia muafaka mbadala ya kupambana na
dawa za kulevya duniani, akidai kutangaza zao
hilo ni haramu kumechangia kukuza biashara
ya bangi kwa njia ya magendo na fedha nyingi
kuishia mikononi mwa walanguzi.
Wajumbe 50 kati ya 96 wa muungano
unaotawala nchini humo "Broad Front
Coalition" waliafiki na kupitisha rasimu katika
ngazi ya chama hapo jana, Jumatano baada ya
mjadala na malumbano yaliyodumu kwa saa
13.
Shirika la Utangazaji la BBC likiripoti taarifa
kutoka nchini Uruguay linasema: "the
control and regulation of the importation,
exportation, plantation, cultivation, the
harvest, the production, the acquisition, the
storage, the commercialisation and the
distribution of cannabis and its by-products".
Ikiwa suala hilo litakuwa sheria,
watakaoruhusiwa kununua bangi ni wale walio
na umri wa zaidi ya miaka 18, watahitajika
kujiandikisha rasmi na wataweza kununua
gramu 40 kwa mwezi kutoka kwenye maduka
rasmi ya dawa au wanaweza kupanda mimea
isiyozidi 6 majumbani mwao.
Sheria hiyo haitaruhusiwa kwa yeyote mgeni,
asiye raia wa nchi hiyo ya Uruguay.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads