YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumanne, 20 Agosti 2013

BILIONEA WA HOME SHOPPING CENTRE ASHINDIKANA KUTIBIWA

Hakika aliyemmwagia tindikali bilionea
Said Mohamed Saad , alifanya kitendo
kibaya kupitiliza, kwani athari ambazo
amemsababishia ni kubwa kiasi ambacho
hata upatikanaji wa tiba mahsusi umekuwa
wa kutangatanga.
Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali
bilionea Said Mohamed Saad hospitalini.
Gazeti hili linazo taarifa za ndani na zenye
uhakika kuwa Said ambaye ni Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni ya Home Shopping
Centre, amekimbizwa Ujerumani kwa
matibabu zaidi baada ya kushindikana
Afrika Kusini alikopelekwa awali .
Said alimwagiwa tindikali Julai 19 , mwaka
huu, mishale ya saa 2 usiku akiwa kwenye
moja ya maduka yake yaliyopo kwenye
jengo analodaiwa kulimiliki la Msasani
Mall.
Ilielezwa kuwa baada ya kumwagiwa
tindikali, alikimbizwa kwenye Hospitali ya
Ami Wellness Centre iliyopo Masaki , Dar es
Salaam lakini ndani ya kipindi kisichozidi
dakika 60, alichukuliwa na kupandishwa
ndege kupelekwa Afrika Kusini.
Said Mohamed Saad akiwa hospitali.
AFRIKA KUSINI MATUMAINI KIDOGO
Ndugu wa Said aliyeomba hifadhi ya jina
lake gazetini , alisema kuwa akiwa Afrika
Kusini, ilionekana kwamba bilionea huyo
anatakiwa kufanyiwa oparesheni ya uso ili
kuondoa ngozi iliyoathiriwa na tindikali,
vilevile kulifanyia jicho upasuaji .
“Sehemu ya usoni kushuka kifuani upande
wa kulia na mkono wenyewe wa kulia
ndiyo maeneo katika mwili wa ndugu yetu
yaliyoathirika zaidi na tindikali, ” alisema
ndugu huyo wa ndani kabisa kwa sharti la
kutotajwa jina na kuongeza:
“Jicho la kulia lenyewe limepata athari
kidogo, kwani inaonekana wakati
mmwagaji akifanya kile kitendo , yeye
alifumba macho kwa hiyo tindikali
haikuingia ndani ya jicho , iliishia kwa juu .
“Ila kwa vile tindikali ilimwagika kwa wingi
juu kwenye jicho la kulia na kutokana na
ukali wa tindikali aliyomwagiwa ,
imesababisha kutengenezwa kwa mtoto wa
jicho kwa hiyo hawezi kuona mbali.
“Uamuzi wa kumpeleka Ujerumani
uliafikiwa baada ya kujiridhisha kwamba
kule kuna wataalamu kuliko Afrika Kusini.
Oparesheni ya uso kubadili ngozi
iliyoathirika, vilevile kufanya upasuaji wa
jicho na kuliweka sawa ni mambo ambayo
tulijiridhisha yanawezekana Ujerumani.”
AKATAA KUTAJA JINA LA HOSPITALI
Kwa mujibu wa ndugu huyo , Said
aliondolewa Afrika Kusini na kupelekwa
Ujerumani, Agosti 3 , mwaka huu na tangu
hapo taarifa zake zimefanywa siri kubwa ili
kulinda usalama wake .
“Hata wakati nazungumza na wewe kama
mwandishi wa habari , nilijua tu lazima
utaniuliza kuhusu jina la hospitali
aliyolazwa Ujerumani. Ukweli ni kwamba
siwezi kukwambia . Tunafanya hivyo kwa
ajili ya usalama wa ndugu yetu.
“Tukio la kumwagiwa tindikali ni zito sana ,
imeshajionesha wazi namna ambavyo kuna
watu hawampendi, hao maadui wakijua
hospitali aliyolazwa , wanaweza kufanya juu
chini wamfikie na kumdhuru kwa mara
nyingine. Hilo jambo hatutaki kabisa
litokee, ” alisema ndugu huyo .
NDUGU, WATOTO WAKE WAZUIWA
KWENDA UJERUMANI
Habari zaidi zinabainisha kuwa ndugu wa
Said walipanga kwenda Ujerumani
kumtembelea lakini walizuiwa kwa sababu
awamu hii, viongozi wa familia yake
wamezingatia usiri.
“Kuna watoto wake walikwenda Afrika
Kusini na walikuwepo wakati anasafirishwa
kwenda Ujerumani lakini waliambiwa
warudi Tanzania kwa sababu kule
Ujerumani utaratibu umebadilika . Watu
wachache wanaohusika na huduma pamoja
na usalama wake ndiyo pekee
wanaoruhusiwa, ” alisema, akaongeza :
“Wapo ndugu wengine kutoka Saudi Arabia
na Oman , vilevile nao wamezuiwa kwenda
Ujerumani kumwona. Ni katika kuhakikisha
mambo hayawi kama ilivyokuwa Afrika
Kusini, maana kule ilishakuwa hatari ,
ndugu wengine wanaingia wodini ,
wanampiga picha na kusambaza
mitandaoni. Safari hii mambo hayo
hayatakiwi.”
APELEKWA UJERUMANI BAADA YA JK
Imeelezwa kwamba Said alipelekwa
Ujerumani wiki moja baada ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dk .
Jakaya Kikwete kwenda kumtembelea
alipokuwa amelazwa kwenye hospitali moja
nchini Afrika Kusini .
Dk. Kikwete, alikuwa kwenye ziara ya kikazi
nchini Afrika Kusini alipokwenda
kuhudhuria Mkutano wa Nchi Wanachama
wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini ya Afrika
(SADC ), kuhusu pande tatu za umoja huo
(Troika of SADC ), hivyo kupata fursa ya
kwenda kumjulia hali.
MUNGU AMPONYE SAID
Dawati la gazeti hili linamuombea Said
apone kwani alionesha moyo wa ukarimu
kwa familia 655 zilizokumbwa na mafuriko
eneo la Jangwani, Desemba, 2011 kisha
kuhamishiwa Mabwepande , Wilaya ya
Kinondoni, Dar es Salaam.
MTUHUMIWA BADO KUKAMATWA
Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa
Kipolisi, Kinondoni, Dar es Salaam, ACP
Camillius Wambura alisema kwamba jeshi
la polisi linaendelea kufanya kazi kwa
nguvu na umakini mkubwa lakini mpaka
sasa halijafanikiwa kumpata mtuhumiwa .

Source:Globalpublishers

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads