YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumatatu, 19 Agosti 2013

AUNT EZEKIEL AFANYIWA UPASUAJI.

MKALI wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel
amefanyiwa oparesheni ya haraka kwa ajili
ya kuondolewa uvimbe tumboni .
Kwa mujibu wa mtu wa karibu na staa
huyo, Aunt alikuwa akitembea na uvimbe
huo siku nyingi pasipo kujijua hadi
alipougua ghafla wakiwa katika mizunguko
ya kila siku jijini Dar, mwishoni mwa wiki
iliyopita.
“Ghafla alibadilika , hakuwa katika hali ya
kawaida kwani tulikuwa tukipiga stori
lakini nikashangaa mwenzangu anabadilika
kama mtu aliyepandwa na presha hivi.
“Tulilazimika kuahirisha misele yetu,
ikabidi twende Hospitali ya Aga Khan na
ndipo alipogundulika kuwa ana uvimbe
tumboni kisha kufanyiwa upasuaji haraka
sana kwani ulikuwa katika hatua mbaya za
kuleta madhara, ” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo mtu huyo wa karibu ambaye
hakupenda jina lake lichorwe gazetini,
alisema staa huyo anaendelea vizuri.

Source:GlobalPublishers

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads