YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumanne, 20 Agosti 2013

MTANDAO WA UNGA WANASWA.

MTANDAO hatari wa unga nchini Tanzania
umeshanaswa, kwa sasa unafanyiwa kazi
kwa kasi na Kitengo cha Kudhibiti na
Kupambana na Madawa ya Kulevya , chini
ya kamanda wake , Godfrey Nzowa .
Habari njema kuhusu kunaswa kwa
mtandao wa unga , zinakuja baada ya
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison
Mwakyembe kufanya kazi nzuri na kuwataja
watu ambao inadaiwa walihusika katika
kupitisha madawa ya kulevya Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA) , Dar es Salaam.
Sekeseke kuu ni kukamatwa kwa
Watanzania wawili , Agnes Gerald
‘Masogange’ ambaye ni mwanamitindo na
Melisa Edward, nchini Afrika Kusini ,
wakiwa na madawa ya kulevya aina ya
Crystal Methamphetamine , yenye uzito wa
kg 120, Julai 5 , mwaka huu.
Swali kwamba walipitaje JNIA lilijibiwa na
Mwakyembe Jumamosi iliyopita , akafafanua
namna Mfumo wa Kamera za Usalama
(CCTV ), zilivyonasa ‘uhuni’ uliofanyika,
hivyo akawataja watumishi wa Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege ( TAA), Yusuf Daniel Issa ,
Jackson Manyonyi , Juliana Thadei na
Mohamed Kalungwana kuhusika, akaagiza
wafukuzwe kazi na polisi kuwakamata.
Baada ya Mwakyembe, moto unaendelea
kuwaka na uchunguzi wa gazeti hili
umebaini kuwa mtandao ulionaswa na
Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na
Madawa ya Kulevya , unagusa mikoa yote
nchini.
Katika mtandao huo, siri kubwa iliyovuja ni
majina na jinsi biashara hiyo haramu
inavyoendeshwa mkoa kwa mkoa, wilayani
mpaka mitaani, vilevile wanamichezo na
wasanii mbalimbali ambao imeshabainika
kwamba wengi wao wanatumika kusafirisha
unga.
Imebainika kwamba mtandao huo,
uligundulika baada ya watu 2, 075
kukamatwa katika kipindi cha Januari hadi
Juni mwaka huu ( baadhi yao, picha zao
zinaonekana ukurasa wa mbele) .
“Watu tuliowakamata kimsingi ni wale
wanaotumwa tu . Sasa wale ndiyo
wamewataja mabosi wao , wameeleza siri
kubwa, ” alisema Kamanda Nzowa na
kuongeza:
“Haikuwa kazi rahisi, tulitumia mbinu za
kiaskari kuwafanya waeleze ukweli.
Wamesimulia biashara hiyo inavyofanyika ,
jinsi watu wenye fedha wanavyowatumia
vijana kusafirisha mizigo .
“Tulichobakiza sasa ni kuwakamata
wahusika na kuusambaratisha mtandao
wenyewe. Hata sasa tunachokifanya ni
kupambana na huo mtandao wenyewe,
mwisho tutausambaratisha kabisa .”
NI MWAKA WA VITA NZITO
Nzowa, alisema kuwa mwaka huu
umeonekana kuwa na vita nzito kwa
sababu kuna lindi kubwa la watu ambao
wamejiingiza katika biashara ya madawa ya
kulevya licha ya wengi kukamatwa na hata
baadhi yao kunyongwa katika nchi za China
na Pakistan .
Alisema madawa ya kulevya yenye uzito wa
kilo 16 ,824 (tani 16.8 ) yamekamatwa kati
ya kipindi cha Januari na Juni, mwaka huu,
idadi ambayo ni kubwa kuliko vipindi
vyote vilivyopita .
Alifafanua kwamba wingi huo usitafsiriwe
tu kwamba biashara ya madawa ya kulevya
inatanuka nchini, isipokuwa itazamwe kwa
jicho la pili kwa upana wake jinsi
mapambano dhidi ya biashara hiyo
yalivyochochewa makali.
“Udhibiti umekuwa mkubwa sana .
Isichukuliwe tu kwamba biashara inazidi
kushika kasi, hapana, haya ni matunda ya
kazi ya udhibiti ambayo inafanyika .
Pengine huko nyuma walikuwa
wanapishana kwa wingi zaidi lakini
mapambano yalikuwa dhaifu , kwa hiyo
wafanyabiashara hiyo haramu walikuwa
wanajitanua tu.
“Ni wajibu wa kila mtu kumwambia
mwenzake aachane na hii biashara ,
tunapomkamata na ushahidi , hapo
anakuwa amekwenda na maji, ” alisema
Nzowa.
Akichambua zaidi , Nzowa alisema takwimu
za madawa ya kulevya aina ya heroin
zilizokamatwa katika kipindi hicho ni kilo
30 na washitakiwa ni 45 , kati yao
wanawake ni wanne .
Alisema, cocaine walikamata kilo nne na
watuhumiwa ni 18 ambao ni wanaume
watupu na dawa aina ya ephedrine
walikamata kilo 12 mshitakiwa ni mmoja
mwanaume na bangi ilikamatwa kilo 9 ,999
na watuhumiwa ni 1 , 478, kati yao
wanawake ni wawili .
Aliongeza kuwa licha ya kukamata bangi,
polisi waliweza kuharibu ekari 300 za
mmea huo katika mikoa ya Arusha , Tanga
na Mara wilayani Tarime .
Kamanda Nzowa akaongeza kwamba polisi
wanafanya kazi hiyo nzuri kwa kushirikiana
na raia wema.
“Hivi sasa tuko makini sana kwa wasanii na
wanamichezo wanaotaka kusafiri kwenda
nje ya nchi kwa sababu tumegundua kuwa
wanatumika kutokana na umaarufu wao ,”
alisema Nzowa .
Akifafanua zaidi , kamanda huyo alisema
wana taarifa kwamba hivi sasa kuna dawa
za kulevya za majimaji , hivyo wanaofikiria
kusafirisha hizo kwa njia hiyo wanapaswa
kujua kuwa watagundulika .
“Hii ni vita ambayo kila anayelitakia mema
taifa hili anapaswa kushiriki kupambana na
dawa za kulevya,” alisema Kamanda Nzowa .
KWA NINI VIJANA WENGI WANAKIMBILIA
UNGA?
Mtafiti maarufu na mwelimishaji wa
maisha ya vijana na jamii kwa jumla, James
Mwang’amba, alisema kuwa vijana wengi
wanaingia katika wimbi la biashara ya
madawa ya kulevya kwa sababu ya kukata
tamaa.
“Ukifuatilia maisha ya vijana kwa sasa,
utagundua kwamba wengi wao wamekata
tamaa. Wanahisi hawana njia ya kutoka
kimaisha ndiyo maana wanaona fursa
yoyote inayokuja mbele yao inafaa hata
kama ni hatari .
“Kila mtu anatamani sana maisha ya juu ,
awe na kipato kikubwa , sasa kwa vile haoni
njia nzuri za kufikia ndoto zake , anaamua
kujiingiza kwenye usafirishaji wa madawa
ya kulevya ili apate fedha za haraka ili naye
awe mtu fulani, ” alisema Mwang’amba na
kuongeza:
“Tatizo kubwa ni hii tofauti ya kipato . Kuna
tofauti kubwa sana kati ya wenye nacho na
wasio nacho , hii ni hatari sana. Sasa jamii
kwa vijana ni hatari zaidi kwa sababu damu
inachemka na kuona kila kitu ni rahisi
kufanya.
“Hakuna sababu nyingine kwa nini vijana
wengi wanakuwa wauza unga , ukweli ni
tamaa ambayo inachochewa na hasira ya
kuwa na maisha duni wakati wanawaona
wengine wakiwa matajiri wakubwa. ”

Source:Globalpublishers

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads