YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumapili, 18 Agosti 2013

Arsenal yaanza vibaya EPL.


Arsene Wenger akiwa amechanganyikiwa baada ya kipigo cha Villa.
Arsene Wenger akiwa amechanganyikiwa baada ya kipigo cha Villa.
Mwanzo wa ligi kuu ya England umekuwa mchungu kwa washika bunduki wa Emirates Arsenal The Gunners baada ya kuanza kwa kipigo toka kwa Aston Villa .
Villa wamewafunga Arsenal 1-3 katika mchezo ambao vijana wa Arsene Wenger walijikuta wakimaliza pungufu uwanjani baada ya beki Laureant Kscielny kuonyeshwa kadi nyekundu.
Arsenal walianza mchezo huo kwa kasi wakifunga mapema kwenye dakika ya siya mchezo , bao hilo halikudumu kwa muda mrefu kwani Aston Villa walirudi mchezoni na kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji Christian Benteke . Mwamuzi Anthony Taylor aliwazawadia Villa penati baada ya kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny kumchezea vibaya Gabriel Agbonlahor . Christian Benteke alipiga penati iliyookolewa na kipa wa Arsenal lakini Mbelgiji huyo alifunga kwa kuufuata mpira wa pili .
Christian Benteke akifunga bao la kwanza kwa Aston Villa.
Christian Benteke akifunga bao la kwanza kwa Aston Villa.

Olivier Giroud alianza kuifungia Arsenal bao kwenye dakika ya 6.
Olivier Giroud alianza kuifungia Arsenal bao kwenye dakika ya 6.

Hali ilianza kuwa mbaya kwa Arsenal baada ya Benteke kuifungia Villa bao la pili kwa mkwaju wa penati . Dakika chache baada ya hapo beki Laureant Koscielny alionyeshwa kadi nyekundu kabla ya beki Antonio Luna hajafunga bao la tatu .
Kadi nyekundu ya Koscielny itawagharimu Arsenal ambao watalazimika kuchezesha mlinzi toka timu ya vijana kama kocha wa Arsenal hatakuwa amesajili beki mwingine mpaka kufikia wikiendi ijayo wakati mchezo mwingine utakapokuwa unapigwa nah ii ni kutokana na mlinzi mwingine wa klabu hiyo Thomas Vermalaen kuwa majeruhi .
Daniel Sturdige akifunga bao la pekee la Liverpool .
Daniel Sturidge akifunga bao la pekee la Liverpool .
Katika mchezo mwingine uliokuwa wa kwanza kwa msimu huu Liverpool wlaiwafunga Stoke City kwa matokeo ya 1-0 . Mchezaji ambaye ameweka historia ya kuwa mfungaji wa bao la kwanza la msimu wa 2013/2014 alikuwa mshambuliaji Daniel Sturidge akifunga bao hilo kwenye dakika ya 37.
Kipa mpya wa Liverpool ambaye alikuwa anacheza mechi yake ya kwanza ya Ligi ndani ya Jezi ya Liverpool Simon Mignolet alikuwa shujaa kwa timu yakje baada ya kuokoa mkwaju wa penati kwenye dakika ya 87 .
Kipa wa Liverpool Simon Mignolet akiokoa penati ya Jonathan Walters
Kipa wa Liverpool Simon Mignolet akiokoa penati ya Jonathan Walters
Katika mchezo wa mwisho kwenye ligi hiyo Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Manchester United walianza vyema utetezi wa taji lao baada ya kuwafunga Swansea City . Mabao mawili mawili toka kwa washambuliaji Danny Welbeck na Robin Van Persie yalitosha kuwapa United matokeo ya 4-1 huku Wilfred Bony akifunga bao pekee kwenye mchezo wake wa kwanza wa ligi akiwa na Swansea . Mshambuliaji ambaye amekuwa akitajwa kwenye tetesi za usajili Wayne Rooney alianza mchezo huo akiwa benchi ambapo aliingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya kocha mchezaji Ryan Giggs.
Robin Van Perise akifunga bao lake la kwanza la msimu.
Robin Van Perise akifunga bao lake la kwanza la msimu.

Wayne Rooney akitokea bench kuchukua nafasi ya Giggs.
Wayne Rooney akitokea bench kuchukua nafasi ya Giggs.

David Moyes akifuatilia mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya England kama Kocha wa Man United.
David Moyes akifuatilia mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya England kama Kocha wa Man United.


Matokeo  ya EPL leo.
Liverpool 1-0 Stoke City .
Arsenal 1-3 Aston Villa.
Norwich City 2-2 Everton.
Sunderland 0-1 Fulham.
West Brom 0-1 Southampton.
West Ham 2-0 Cardiff City.
Swansea City 1-4 Manchester United.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads