YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumamosi, 6 Julai 2013

RAIS KIKWETE MGENI RASMI TAMASHA LA MATUMAINI KESHO

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania, Jakaya Kikwete .
RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania , Jakaya Kikwete , ndiye mgeni
rasmi katika Tamasha la Usiku wa
Matumaini, linalotarajiwa kufanyika kesho,
Uwanja wa Taifa , Dar es Salaam.
Uthibitisho huo kwamba JK atakuwa mgeni
rasmi unatoa picha kwamba Usiku wa
Matumaini ni tamasha la kitaifa , lenye
maana kubwa kwa Watanzania .
Akiwa uwanjani hapo rais atatoa hotuba ya
matumaini kwa Watanzania, lengo likiwa ni
kuamsha hamasa kwa wananchi kuipenda
na kuitumikia nchi yao ili kulifanya taifa
kuwa la amani na lenye mafanikio
makubwa kiuchumi .
Baada ya neno hilo , JK atakagua timu za
wabunge wa Simba na Yanga na baadaye
kupuliza kipyenga kuashiria kubariki
mchezo huo unaosubiliwa kwa hamu na
mashabiki wa timu hizo kongwe nchini .
Mechi hiyo ya wabunge wa Simba na
Yanga, mwaka huu imeongezewa nguvu
baada ya viongozi wa timu hizo
zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara
kuamua kuwaongeza baadhi ya wachezaji
tegemeo kutoka kwenye vikosi vyao kwa
lengo la kuweka msisimko wa mechi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads