YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumamosi, 6 Julai 2013

CD YA DIAMOND YAUA MTOTO

VILIO, simanzi, huzuni vilitanda Jumatano
iliyopita Mwananyamala Kisiwani , jijini Dar
kufuatia mtoto wa mwaka mmoja , Rahim
Rajab kufariki dunia kwa kuangukiwa na
watu watatu , akiwemo baba yake mzazi,
Rajab Said, Risasi Jumamosi lina mkanda
wote.
Tukio la watu hao kumwangukia mtoto
huyo lilitokea Jumatatu iliyopita na
lilisababishwa na ugomvi mkubwa wa CD
yenye nyimbo za mwanamuziki wa Bongo
Fleva , Nasibu Abdul ‘ Diamond’ ulioibuka
ndani ya chumba cha kulala kati ya mama
wa marehemu na mpangaji mwenzake
aitwaye Aisha.
MAZINGIRA YA TUKIO
Akizungumza kwa machungu kuelezea tukio
hilo, mama mzazi wa marehemu Rahim,
Habiba Ally alikiri kuwa kisa cha kifo cha
mwanaye ni CD tu.
Akasema : Kwa kweli hakuna kingine zaidi
ya CD , naamini hivyo kwa kuwa mimi
sikuwa na ugomvi wowote na Aisha.
Tulikuwa tunaishi kawaida tu ukiacha
mikwaruzo ya hapa na pale. ”
Akaongeza : Jumamosi iliyopita , Aisha
alikuja ndani kwangu na CD zake tatu, ya
Diamond, Kingwendu na ya Coast Modern
Taarab. Alipomaliza kuangalia aliziacha ,
akaondoka zake .
“Jumapili mimi nikaenda nazo kwa mama
zote tatu kwa ajili ya kuziangalia,
tulipomaliza na mimi niliziacha huko .
“Jumatatu usiku Aisha akaja kunidai,
nikamwambia zipo kwa mama . Kwa kuwa
anapajua anapoishi mama, si mbali
akaenda kuzichukua zote tatu . Ajabu
aliporudi tu, akaja tena kwangu na kusema
hajapewa CD ya Diamond kitu ambacho si
kweli na ndipo ulipozuka ugomvi wote huo
hadi kusababisha kifo cha mwanangu.”
BIBI WA MAREHEMU SASA
Akizungumza na Risasi Jumamosi msibani
juzi, bibi wa marehemu, Jamima Hassan
alisema siku ya tukio alipigiwa simu na
mkwe wake (baba wa marehemu)
akamwambia kuna ugomvi nyumbani
kwake unaohusu CD kati ya mkewe na
mpangaji mwenzake ambapo bibi huyo
aliamua kwenda kutatua ugomvi huo .
“Niliondoka muda huohuo kwani huyo
Aisha alitoka kwangu kuchukua CD zake
muda mfupi tu, sasa nilijiuliza ni CD gani
wanazogombania?
“Nilipofika nilikuta ugomvi umepamba
moto, baba wa mtoto na mume wa Aisha
aitwaye Shaban Sangali walikuwa
wameungana kumtoa nje ya chumba Aisha
bila mafanikio .
“Wakati naingia, Aisha alikuwa akitukana
matusi mazito na tulipojitahidi kumtoa nje
alitusukuma kwa nguvu. Ndipo yeye,
mume wake na baba wa mtoto
waliwaangukia watoto waliokuwa wamelala
kitandani,” alisema bibi huyo .
Akaendelea: Tulipowaangalia watoto ambao
ni mapacha, hali zao zilikuwa mbaya ,
tukaamua kwenda kwa mjumbe wa mtaa
kuripoti, akatupa barua, tukaenda Kituo
cha Polisi Mwinyijuma , pale wakatupa PF3
ya kuwapeleka Hospitali ya Mwananyamala
ambako walilazwa kwa matibabu.
Bibi huyo alisema siku iliyofuata , Rahim
alifariki dunia , ikabidi waende Polisi
Oysterbay ambapo walifungua shitaka
lenye faili kwa kumbukumbu No . OB /
RB/ 1150 /2013 MAUAJI.
Watuhumiwa katika RB hiyo ni Aisha na
mumewe, Sangali ambao walikamatwa na
kufikishwa kituo cha polisi.
ILIVYOELEZWA NA MAJIRANI
Majirani waliozungumza na gazeti hili
walisema wakati ugomvi kati ya Aisha na
Habiba unatookea , mume wa Habiba
alikuwa anarudi kutoka kazini , akakutana
na kimbembe hicho.
Walisema aliingilia kati kuamua bila
mafanikio. Wakati huo mume wa Aisha
alikuwa chumbani kwake na amefungulia
muziki wa redio kwa sauti ya juu hivyo
hakujua nini kinaendelea kwenye chumba
cha mpangaji mwenzake.
Ikaelezwa kuwa , kuna watu walikwenda
kumgongea na kumwambia mkewe
anapigwa na mume wa Habiba kwa
kushirikiana na mkewe .
Ilibidi mwanaume huyo atoke mbio hadi
chumbani kwenye ugomvi ambako alikuta
baba wa marehemu akijitahidi kuwaamulia
wawili hao bila mafanikio.
Habari zinasema mwanaume huyo aliingilia
kati kuongeza nguvu lakini katika hali ya
kuwalemea, Aisha aliwasukuma wote na
kisha wao kuwaangukia watoto hao
mapacha waliokuwa wamelala kwenye
kitanda kimoja .
RAHIM AMEMUACHA RAHIMA
Katika hali ya kusikitisha, marehemu
amemuacha pacha mwenzake aitwaye
Rahima Rajab ambaye ni kulwa.
Wengi wanaamini kuwa maisha ya Rahima
yangekuwa ya furaha zaidi kama Rahimu
angekuwepo na kwamba itamsononesha
sana akikua na kusikia mwenzake alifariki
dunia kwa ugomvi wa mama yake na
mpangaji mwenzao kisa ni CD ya nyimbo za
mwanamuziki.
NENO LA MJUMBE
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kisiwani
aliyejulikana kwa jina moja la Mtawa
alipoongea na gazeti hili alisema
amesikitishwa na tukio hilo la kuuawa kwa
mtoto Rahim na kuongeza kuwa ni vema
wazazi wakawa makini na watoto wao ili
matukio ya kushitua kama haya yasitokee.
Alikiri kumfahamu Aisha na kusema kuwa
mara nyingi amepokea malalamiko dhidi
yake na amekuwa akimtaka kuishi vizuri na
majirani wenzake bila mafanikio

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads