YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Ijumaa, 21 Juni 2013

Ugeni wa David Beckham nchini China wazua maafa baada ya umati wa mashabiki kukanyagana wakati wa mapokezi

Mashabiki wa mchezaji mstaafu wa
Uingereza David Beckham wamejeruhiwa
katika vurugu zilizotokea wakati wa mapokezi
ya nyota huyo nchini China. Beckham yuko
China kwa ziara ya wiki moja akiwa kama
balozi wa soka la nchi hiyo.
Kwa mujibu wa The Guardian watu wapatao
saba walijeruhiwa baada ya umati wa
mashabiki wapatao 1000 kusukumana wakati
wa mapokezi ya star huyo katika chuo cha
Tongji nchini China. Kati ya waliojeruhiwa
wamo maaskari watatu, walinzi wa chuo cha
hicho wawili na wanafunzi wawili.
Inasemekana umati huo mkubwa ulikuwa
umekusanyika katika uwanja wa chuo hicho
ambapo Beckham alipangiwa kwenda
kukutana na team ya chuo. Baada ya vurugu
hizo kutokea zoezi zima lililokuwa
limepangwa liliahirishwa.
Wakati Beckham anawasili uwanjani hapo
mashabiki hao waliokuwa na kiu cha
kumuona kwa karibu walivamia geti na
kuwazidi nguvu walinzi wa uwanja pamoja na
maaskari, kitendo kilichopekea mkanyagano
uliosababisha watu kujeruhiwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads