YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Ijumaa, 21 Juni 2013

RAIS MSTAAFU GEORGE BUSH ATATUA JIJINI DAR ES SALAAM MWEZI UJAO

Rais mstaafu wa Marekani, George W.
Bush na mkewe, Laura, wanatarajiwa
kuwasili nchini mwezi ujao ambapo
watahutubia kongamano litakalojadili wajibu
wa wake za marais katika kuinua wanawake
duniani.
Taasisi ya George Bush ndiyo imeandaa
kongamano hilo litakalofanyika Dar es Salaam
kuanzia Julai 2 hadi 3.
Taarifa iliyotolewa jana na taasisi hiyo kwa
vyombo vya habari, ilisema kongamano hilo,
litahudhuriwa pia na mke wa Rais Barack
Obama wa Marekani, Michelle na muasisi
wa Taasisi ya Wanawake ya Cherie, Cherie
Blair ambaye ni mke wa Waziri Mkuu wa
zamani wa Uingereza, Tony Blair.
Wake wengine wa marais wa Afrika
watakaohudhuria ni Mama Salma Kikwete,
Chantal Campaore wa Burkina Faso, Roman
Tesfaye wa Ethiopia, Maria da Luz Dai
Guebuza (Msumbiji), Penehupifo Pohamba
(Namibia), Sia Nyama Koroma (Sierra Leone),
Janet Museveni (Uganda) na Christine Kaseba
wa Zambia.
Kongamano hilo litajikita zaidi katika kujadili
masuala ya kuwekeza kwa wake, kuimarisha
Afrika lakini pia wajibu wa wake za marais
kuhamasisha wanawake katika maeneo ya
elimu, afya na kuwakwamua kiuchumi.
“Kongamano hili litakutanisha pamoja
wake za marais, maofisa wa Serikali,
mashirika binafsi, Asasi Zisizo za Serikali
(AZISE) na wasomi kujadili mambo muhimu
ya kuchukuliwa hatua ili kunufaisha
wanawake,” ilisema taarifa hiyo.
Aidha, mada zitakazowasilishwa na kujadiliwa
katika kongamano hilo ni kuinua wajasiriamali
wanawake kiuchumi kupitia mafunzo na
teknolojia, kupatia fursa wanawake wakulima
kwa kupewa mafunzo ya kilimo cha kisasa,
mafunzo kuhusu saratani ya matiti na
umuhimu wa elimu kwa wanawake.
Kongamano hilo linafanyika sambamba na ujio
wa Rais Obama anayetarajiwa kuwasili nchini
mwanzoni mwa mwezi ujao.
Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika
ambazo kiongozi huyo atazuru katika ziara
itakayoanza Juni 26 hadi Julai 2. Nchi nyingine
ni Senegal na Afrika Kusini.
Ziara za kiongozi huyo na Bush, inafanya
Tanzania mwaka huu kushuhudia ugeni wa
watu mashuhuri mfululizo, baada ya Rais Xi
Jiping wa China Machi 28, ambapo Tanzania
ilikuwa nchi ya kwanza kutembelea Afrika
tangu achaguliwe kuwa Rais Machi 14.
Amani, utulivu na uimara wa mfumo wa
demokrasia ni miongoni mwa mambo
yanayotajwa kuvutia viongozi hao wa kimataifa
kuja nchini.
Wapo wengine ambao katika maoni yao juu
ya ujio wa viongozi hao, wamekuwa wakisema
ugunduzi wa rasilimali za asili kama vile gesi,
mafuta na madini ya urani ni sababu nyingine
ya Tanzania kutembelewa.
Hata hivyo, Balozi wa Marekani nchini,
Alfonso Lenhardt alikaririwa hivi karibuni
akifafanua, kwamba ziara ya Obama haina
ajenda yoyote ya kuchukua rasilimali za
Tanzania, bali ni ya uhusiano wa kiuchumi kati
ya nchi hizo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads