YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumatatu, 10 Juni 2013

STAR TV YATANGAZA KUJITOA KATIKA VING'AMUZI VYA STAR TIMES......TCRA YAGOMA NA KUDAI KUWA SHERIA HAIRUHUSU KUJITOA

BAADA ya Televisheni ya Star TV
kutangaza kujitoa kurusha matangazo yao
kupitia kingamuzi cha Star Times,
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) imesema sheria na leseni ya
huduma, inazuia kuchukua hatua hiyo.
Hata hivyo, TCRA imesema inafanya
uchunguzi na leo itakutana na uongozi wa
Star TV na Star Times, kuzungumzia suala
hilo ili hatua za udhibiti, zichukuliwe
kuwezesha wananchi kupata haki ya
msingi ya kupata matangazo ya kitaifa
kupitia televisheni hiyo.
Star TV walitangaza kutoonekana kupitia
Star Times siku chache zilizopita.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa, jana
waliwasilisha barua ya hatua hiyo kwa
kampuni ya Star Times kupitia
mwanasheria wa kampuni yao.
Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent
Mungy aliliambia HabariLeo jana kuwa
na wao wamesikia taarifa hiyo kupitia
vyombo vya habari Lakini, alisema Sheria
ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta
(EPOCA) ya mwaka 2010, haitoi fursa kwa
watu wenye televisheni kujitoa ama
kujiweka kwenye ving’amuzi watakavyo.
“Kwa ujumla chaneli zile tano za kitaifa,
zinapaswa kuonekana bure kwenye
ving’amuzi vyote, nasi tumesikia habari
hizi na lazima tufanye uchunguzi, lakini
pande zote mbili pamoja na sheria, pia
wanafungwa na mkataba wa huduma kwa
jamii na matakwa ya leseni,” alisema
Mungi na kuongeza:
“Sheria inawataka wawe na
makubaliano, huwezi kusema mimi
najitoa, leseni ina matakwa yake lazima
yafuatwe. Lakini kesho (leo) tutawaita
kujua kilichotokea ni nini na hatua zaidi
zitachukuliwa baada ya hapo”.
Aliwahakikishia wananchi ni haki yao
kupata matangazo kupitia televisheni ya
Star TV, hata bila kulipia ving’amuzi,
kama ilivyo kwa televisheni nyingine nne
za ITV, TBC, Channel 10 na EATV.
Msaidizi wa Meneja wa Star Times, Hellen
Elisa alithibitisha kujitoa kwa Star TV.
Alieleza ni kweli walipokea barua mbili
juzi, zikieleza kuhusu hatua yao hiyo
kwamba wamejitoa kwa matakwa yao.
“Walituletea barua jana (juzi) kupitia
mwanasheria wao wa kampuni, wao ni
wamiliki wa chaneli, na sisi tunahusika
kurusha matangazo, jambo lolote kama
hili likitokea lazima kwanza kutii sheria,
tumewasiliana na TCRA na wakubwa
wetu wa kazi wametueleza kuwa
wanalishughulikia kwa karibu,” alisema
Elisa.
Kwa upande wake, Msimamizi wa masuala
ya Ving’amuzi wa Sahara Media Group,
wamiliki wa Star TV, Steve Diallo
alipoulizwa kwa simu kuhusu kujitoa kwao
Star Times, alisema yeye si Msemaji na
kumtaka mwandishi kuwasiliana na watu
wengine.
Miezi kadhaa iliyopita, Clouds TV nayo ilijitoa,
lakini ikarejea tena. Jana, Mkurugenzi wa
Utafiti wa Redio Clouds FM, Ruge Mutahaba
alisema sheria inawabana wamiliki wa
televisheni za kijamii kujitoa na wanapaswa
kuonekana katika ving’amuzi vyote.

SOURCE: HABARI LEO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads