YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumamosi, 29 Juni 2013

NELSON MANDELA UJANA MPAKA UZEE , GEREZANI ALITUMIA BLANKETI KUTOKA TANZANIA

RAIS Mstaafu wa Afrika Kusini , Mzee
Nelson Mandela ( 94) hali yake kiafya bado
tete kwa maradhi ya mapafu na ini
yanayomsumbua, hivi sasa amelazwa katika
Hospitali ya Mediclinic Heart jijini
Pretoria, Afrika Kusini.
Mzee Mandela au maarufu kama Madiba
historia ya maisha yake ni ndefu, lakini leo
katika safu hii tunapenda kushughulika na
picha zinazomuonesha akiwa katika vipindi
mbalimbali katika maisha yake.
Ila kwa ufupi sana , Mzee Madiba alikuwa
mpinzani wa serikali ya kibaguzi nchini
mwake , matokeo yake alifungwa maisha
katika Gereza la Kisiwa cha Robben lakini
akatumikia miaka 27.
Akiwa gerezani , kuna taarifa kuwa Mzee
Madiba alitumia blanketi lililotengenezwa
nchini Tanzania lenye chapa ya Super
Simba na picha ya mnyama huyo (angalia
picha).
Kifungo chake kilitokana na kupatikana na
hatia ya kuhujumu na kula njama ya
kuipindua serikali ya Makaburu . Aliachiwa
huru mwaka 1990 . Mei 10 , 1994
akachaguliwa kuwa rais wa nchi yake akiwa
Mwenyekiti wa Chama cha African
Congress Party. Juni 14 , 1999 aliacha
kugombea nafasi hiyo.

Source: Global Publishers

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads