YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Ijumaa, 21 Juni 2013

MAKAMPUNI YA SIMU KUPANDISHA GHARAMA KUANZIA JULAI MOSI

Kufuatia kuongezwa kwa kodi katika
huduma za simu za mkononi , gharama za
huduma hizo zinatajiwa pia kuongezeka
kuanzia Julai Mosi mwaka huu.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa jijini Dar es
salaam na Umoja wa Makampuni ya Simu
za Mkononi Tanzania – MOAT imesema
pendekezo la serikali la kuweka kodi ya
14.5 kwenye huduma za simu za mkononi
hazotoweza kukwepesha kupanda kwa
gharama za simu kwa watumiaji .
MOAT inasema awali kodi ilikuwa ikitozwa
asilimia 12 .5 katika huduma ya
mawasiliano ya simu na kwmaba ongezeko
la kufiikia asilimia 14 .5 tofauti na nchi za
jirani Kenya na Uganda ambazo
zimeendelea kutoza viwango vya ushuru
vya asilimia 10 na 12 .5 tu ni mzigo kwa
watumiaji wa huduma za simu za mkononi.
Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka
2013 unaainisha, huduma za mawasiliano
kuwa ni; “huduma yoyote ya maelezo
inayotolewa na makampuni ya mawasiliano
ya simu kwa njia ya mawasiliano kwa kutoa
au kupokea sauti, maandishi , na picha au
taarifa ya aina yoyote kupitia mfumo wa
kielektronikia. ”Imesema taarifa hiyo
iliyosainiwa na Vodacom , Airtel, Tigo na
Zanztel
MOAT imesema eneo mojawapo
litakaloathirika ni huduma za Intaneti eneo
amablo linahitaji kuwekewa mikakati ya
kulikuza kutokana na umuhimu wake katika
maisha ya sasa kiuchumi na kijamii na wala
sio kulizorotesha kwa kusababisha
ongezeko la gharama na hivyo kuendelea
kuwa na kiwango cha cha matumizi
kilinganishwa na baadhi ya nchi nyengine
zikiwemo za Afrika Mashariki.
“Hatua hii ya kuongeza kodi itakwenda
kinyume na mipango iliyopo yenye lengo la
kuibadili jamii kwa kuipatia maarifa ya
msingi kupitia huduma ya intaneti
sambamba na mawasiliano ya simu .”
Kwa mujibu wa MOAT, Tanzania ni kati ya
nchi zenye kiwango cha chini ya matumizi
ya huduma ya mtandao wa intaneti katika
bara la Afrika ambapo watumiaji wa
huduma hiyo ni asilimia 10 pekee
ikilinganishwa na nchi jirani ya Kenya
ambayo ina zaidi ya watumiaji asilimia 40 .
Aidha, MOAT imeongeza kuwa ,
“mawasiliano ya simu si anasa bali ni
huduma muhimu katika Tanzania ya leo ,
sasa tunawezaaje kuwatozakodi mara kwa
mara watu hao hao ambao wanaitegemea
huduma hiyo ili kuboresha maisha yao?
Ilihoji taarifa hiyo ya MOAT .
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa kwa
tozo la kodi ya mapato ya asilimia 35
kwenye sekta hiyo ya mawasiliano ya simu
linatosha kiasi ya kwamba sekta hiyo
isngeweza kubeba mzigo zaidi wa ongezeko
jingine.
Hivi sasa , upanuzi wa mawasiliano na
miundombinu vijijini ndiyo kipaumbele cha
sekta nzima. Tunaamini hapa ndipo ukuaji
wa sekta ya mawasiliano ya simu
itakapoonekana katika miaka ijayo.
Ongezeko lolote la kodi litazorotesha
uwezo wetu wa kutanua huduma zetu za
mawasiliano na miundombinu maeneo ya
vijijini, imesema MOAT .
“Tunaelewa kuwa serikali inayafanya haya
yote ili kuweza kupata fedha kwa ajili ya
kusaidia kwenye huduma za jamii katika
maeneo muhimu . Ni bahati mbaya kwamba
sekta ya huduma ya mawasiliano ya simu
inaendelea kubeba mzigo mkubwa wa
ongezeko hili ambapo wateja watalazimika
kuubeba mzigo wa ongezeko hilo ,”
ilihitimisha taarifa hiyo ya MOAT .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads