YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumanne, 25 Juni 2013

MAAJABU: MWANAMKE AMEOA WANAUME WAWILI NA KUISHI NAO...!! SOMA HAPA

MWANAMKE mkazi wa kijiji cha
Ikandamoyo, wilayani Katavi, Veronica
Saleh ‘Mama Kaela’ (50), amefanya
uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume
wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.
Kijiji hicho kipo umbali wa takribani
kilometa 30 kutoka mjini hapa katika
Jimbo la Katavi linalowakilishwa na
Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Pamoja na ndoa hiyo iliyowezeshwa na
mume mkubwa kukubali kuishi na mume
mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo
ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa
zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na
amri kuu katika nyumba, kama ilivyo
katika ndoa za kawaida.
Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba
Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa
na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume
mdogo.
Taarifa za kuwapo kwa ndoa hiyo ya
aina yake, ziliifikia Globu ya Jamii na
kufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki
tatu, na hatimaye katikati ya wiki hii,
wahusika walikubali wao wenyewe
kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu wa
maelezo ya mwanamke huyo ambaye
alionekana kuwa msemaji wa familia
hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika
kijijini hapo miaka 24 iliyopita, wakitoka
kijiji cha Usumbwa mpakani mwa
Chunya, Mbeya na Tabora.
Wakiwa kijijini hapo mume wake
aliendelea kufanya kazi ya ukulima
wakati yeye mama (Veronica), pamoja
na kilimo hujihusisha na upishi na
uuzaji wa pombe ya kienyeji iitwayo
kayoga.
Mwanamke huyo ambaye amesema ana
watoto wanne, Alfred (20), binti mwenye
miaka 16 (ambaye ameolewa) na wengine
wawili wa kiume, mmoja akisoma
darasa la sita na mdogo ana miaka
saba, amesema hana shida na waume
wake.
Ingawa wanandoa hao walizungumza
kwa hadhari, majirani walikiri kuwa
mwanamke huyo anaishi na wanaume
hao wawili kwa amani na kwamba
mwanamke huyo ndiye mwenye sauti na
si waume zake.
“Si siri tena sasa, tumeshawazoea,
kwani wanaishi kwa amani ila yule
mume mdogo anaishi kwenye nyumba
aliyoachiwa na marehemu baba yake,
lakini anashinda kwa mume mkubwa,
ambapo inajulikana kijijini hapa kuwa
ni nyumba kubwa. “Basi pale ni mambo
yote, kula na kunywa, mama huyu
amewapangia zamu wanaume hao kama
afanyavyo mume mwenye wake wengi.
Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona
ya Firauni,” alisema mkazi mmoja kwa
masharti ya jina lake kutoandikwa
gazetini. Ilielezwa, kwamba wanaume
hao wana akili timamu na hawatumii
kilevi cha pombe kama ilivyo kwa mke
wao.
Hata hivyo, mume mkubwa anapewa sifa
za upole tofauti na mume mdogo
anayetajwa kuwa mkorofi kiasi cha
mara kadhaa kumchapa makofi mkewe
anapomuudhi.
Majirani wanadai kwamba Mama Kaela
na mumewe Paulo, walipofika kijijini
hapo, walipokewa na kuishi maisha ya
kawaida, lakini baadaye mama huyo
alianza kuwa na uhusiano wa kimapenzi
na Arcado, ambaye naye alilazimika
kuachana na mkewe wa ndoa
anayefahamika kijijini hapo kwa jina la
Mama Pere.
Ilielezwa na mashuhuda hao kwamba
mume mkubwa alipobaini uhusiano huo,
alikuja juu, lakini mwanamke huyo
inadaiwa alimweleza mumewe huyo,
atake asitake lazima wataishi wawili,
vinginevyo ataachana naye, ndipo mume
mkubwa alipokubali kuishi na mume
mwenza.
Katika maisha ya kawaida katika
familia hiyo, inaelezwa kwamba katika
baadhi ya siku ikitokea kuwa mama
huyo amechoka kupika, mume mdogo
huchukua jukumu la kupika na
kumwandalia chakula na maji ya kuoga
mume mkubwa.
“Lakini mara nyingi kwa mfano, ikiwa ni
zamu ya mama huyo kulala kwa
mumewe mkubwa, basi humfulia nguo
zake kisha anakwenda kwa mumewe
mdogo nako anamfulia nguo.
“Ndivyo wanavyoishi, nasi sasa
tumewazoea ila yule mama ni mkali na
ana sauti pale kwake kwa wanaume wale
ila tunaona kama ana wivu sana kwa
huyu mdogo ambaye naye pia ana wivu
kwa mkewe huyo, labda anahofia kuwa
mama huyo anaweza kuongeza
mwanamume mwingine,” anasema
mmoja wa majirani hao.
Hakuna mazuri yasiyokuwa na
machungu, japo familia hiyo inaelezwa
kuwa na amani, mtoto wao mdogo
nusura avuruge uhusiano wa wanandoa
hao, baada ya kuibuka mzozo wakati wa
maandalizi ya ubatizo wake.
Kwa sababu anazojua mama, ingawa
inafahamika kuwa wote ni watoto wa
mume mkubwa, mke huyo katika hati za
ubatizo aliandikisha ubini wa mtoto
huyo kuwa ni Mlele (akimaanisha kuwa
mtoto wa mume mdogo), lakini mume
mkubwa aliweka pingamizi kanisani
akidai yeye ndiye baba halali wa mtoto
huyo.
Kwa mujibu wa mwanamke huyo, yeye
na Arcado ni waumini wa madhehebu ya
Katoliki wakati Paulo ni Mpentekoste.
Madai ya mzozo wa uhalali wa `ubaba’
wa mtoto huyo, yalithibitishwa na
baadhi ya wakazi wa kijiji hicho,
akiwamo mwalimu wa dini wa Kigango
cha Kanisa Katoliki Uruira, Mashaka
Abel. Walisema miaka sita iliyopita,
mtoto huyo akiwa na umri wa mwaka
mmoja, alifanyiwa taratibu za ubatizo,
lakini ilishindikana, kutokana na
wanaume hao, kila mmoja kudai ndiye
baba mzazi wa mtoto.
“Lilikuwa jambo la kustaajabisha sana,
kwani familia hiyo ilifanya maandalizi
yote ya sherehe ya ubatizo wa mtoto
huyo, lakini siku hiyo kanisani wakati
huo ilikuwa ni kigango cha Katumba
ambacho sasa ni Uruira, sakata lilianzia
pale Padri alipomwuliza mama wa
mtoto huyo ubini wa mtoto naye
akasema ni Mlele.
“Hapo ndipo mume mkubwa alipopinga
na kudai kuwa mtoto yule si wa Arcado
bali wake na yeye ndiye baba halali.
Padri hakuamini, aliuliza tena na tena
na majibu yakawa ni yale yale, ndipo
ubatizo ukashindikana,” alisema
Katekista Abel.
Kazi ya kutafuta undani wa ndoa hiyo
haikuwa rahisi kutokana na mazingira
ya woga na usiri uliokusudiwa kubaki,
ambapo awali mama alisema kwamba
mume wake ni Paulo pekee japo siku
ambayo mwandishi wa habari hizi
alifika kijijini hapo na baadaye
nyumbani kwa wanandoa hao na
kumkuta mume mdogo (Arcado
akimsaidia mkewe kukoroga pombe.
Awali katika utambulisho, walidai kuwa
ni mtu na mdogo wake na kusita
kuzungumzia maisha yao ya kifamilia.
Mke wao ambaye alionekana wazi kuwa
ni msemaji mkuu alifoka na kuja juu,
akidai kuwa hayuko tayari kuzungumzia
uhusiano wake na wanaume hao wawili,
ingawa alikiri kuwa wanaishi pamoja.
"Kwa hiyo umefunga safari yote hii
kutoka huko ulikotoka ili uje kwangu mie
Veronica … nasema sitaki kabisa mtu
kuja hapa na kutaka kunivurugia
mpangilio wa maisha yangu, kwanza
nani alikueleza hayo, wambea wakubwa
hao yanawahusu nini watu hao?” alihoji.
“Mie mume wangu ni huyu Paulo basi …
sasa leo umeniachia vurugu ndani ya
nyumba nitapigwa na huyo mume wangu
Paulo, kwani mmenishikisha ugoni?”
alifoka Mama Kaela. Hata hivyo, mume
mkubwa alidai kuwa hatamwadhibu
mkewe huyo na kwamba wataendelea
kuishi pamoja na mdogo wake Arcado
kwa amani. Hata hivyo, akina mama
wengi kijijini hapo wanalaani kitendo
cha mama huyo kuishi na wanaume
wawili ambapo waliomba uongozi wa
Kanisa uingilie kati, ili mama huyo
aweze kufunga ndoa na mume mmoja.
Lakini kwa upande mwingine, baadhi
walimpongeza mwanamke huyo wakidai
kuwa kitendo hicho ni cha kijasiri kwa
mwanamke, kumudu kuishi na wanaume
wawili na kuwa na mamlaka juu yao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads