YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumanne, 14 Mei 2013

WABUNGE WADAIWA KUPEANA MIMBA

SKENDO nzito inalitafuna Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania , ikitawala madai
kwamba kuna wabunge wawili wanawake ,
wamejazwa mimba na waheshimiwa
wenzao wanaume .
Mbunge wa Mtera ( CCM) , Livingstone
Lusinde .
Awali, ulitawala uvumi kuwa mmoja wa
wabunge wa upinzani ( viti maalum ),
akitokea Kanda ya Kaskazini , amepewa
ujauzito na mheshimiwa mwingine ambaye
ni kiongozi anayeshika nafasi za juu
kwenye moja ya vyama vikuu vya upinzani
nchini (wote majina yao tunayahifadhi kwa
sasa).
Kashfa hiyo ya mtunga sheria huyo kupewa
mimba na mheshimiwa mwenzake ambaye
ni mume wa mtu, ilipata mbeleko na
kuifanya ivume zaidi, baada ya Mbunge wa
Mtera ( CCM) , Livingstone Lusinde , kulipuka
bungeni: “Humuhumu ndani kuna wabunge
wanawake wenye mimba zisizotarajiwa .”
Lusinde, alitamka hayo Aprili, mwaka huu,
wakati akichangia hotuba ya bajeti, Ofisi ya
Waziri Mkuu, kipindi ambacho bunge
lilikuwa limechafuka kutokana na wabunge
kurushiana ‘ mipasho’ wao kwa wao .
Kauli ya Lusinde, pamoja na kupokelewa
tofauti na wabunge wengi wanawake ,
wakidai mheshimiwa mwenzao
amewadhalilisha, upande mwingine , katika
‘vikao vya kwenye korido ’, matukio ya
vicheko na kugonga mikono yalitawala na
kunena kwa msisitizo “ message delivered” ,
yaani ujumbe umefika.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM ) Mkoa wa
Morogoro , Sara Msafiri.
Wakati mwandishi wetu akifuatilia sakata
lenyewe, mbunge mwingine wa Viti
Maalum (CCM ) ambaye jina lake tunaliweka
kabatini, aliamua kufunguka :
“Nashangazwa sana na haya madai,
tunawasema wapinzani , wakati hata kwetu
(CCM ) kuna watu wamepeana mimba .”
Mbunge huyo alisema kuwa siyo siri
mjengoni kuwa mmoja wa watunga sheria
wa CCM, anayetokea moja ya majimbo ya
Kanda ya Magharibi , amempa ujauzito
mheshimiwa mwingine kutoka chama
tawala, anayewakilisha viti maalum ( majina
yao yamehifadhiwa kabatini kwa sasa).
Kwa mujibu wa mtoa habari huyo , mbunge
anayetajwa kupewa mimba , anatokea
kwenye ukoo wa mmoja wa vigogo
waliowahi kushika nafasi za juu kabisa
kwenye Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania .
WABUNGE WASHIKA BANGO
Wabunge mbalimbali waliozungumza na
mwandishi wetu , walikiri kutambua uwepo
wa wenzao wenye uhusiano wa kimapenzi
kiasi cha kufikia kupeana mimba .
Mbunge mwingine alithubutu kutamka :
“Nini hao kupewa mimba na zinaonekana,
wapo ambao wanapata na wanatoa . Yote
hayo tunayajua. ”
Mbunge wa Ubungo ( Chadema ), John
Mnyika.
NANI AMFUNGE PAKA KENGELE?
Katika kufanyia kazi kila
kinachozungumzwa, mwandishi wetu
alizungumza na baadhi ya wabunge
ambapo Mbunge wa Ubungo ( Chadema),
John Mnyika, alisema : Unajua madai ya
mimba yanawahusu wanawake , kwa hiyo
waulizwe wenyewe.
“Kama umenitafuta mimi kwa kigezo
kwamba ni mbunge kijana , basi waulize
wabunge vijana wanawake ,” alisema
Mnyika.
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR -Mageuzi ),
David Kafulila, alikiri kufahamu kuwepo
kwa tuhuma kwamba wapo wabunge
wamepeana mimba lakini hawezi kuwa na
uhakika kwa sababu uhusiano wa
kimapenzi ni jambo la faragha.
“Hayo madai yapo , yanazungumzwa. Wapo
wanaotajwa kuwa na uhusiano wa
kimapenzi, hayo ni mambo ya faragha .
Sijui pengine walioanzisha haya madai
wana vipimo vyao ,” alisema Kafulila.
VIPI MIMBA ZISIZOTARAJIWA NA UTOAJI?
Mbunge wa Viti Maalum (CCM ) Mkoa wa
Morogoro, Sara Msafiri, alisema kuwa
haiwezekani wabunge kupata mimba
zisizotarajiwa kwa sababu ni watu wazima .
“Wabunge tunapata mafunzo ya uzazi , kwa
hiyo kama ni mimba basi mtu anakuwa
amepanga kuipata. Hakuna kitu kama
hicho. Hata hilo la kutoa mimba halipo
kabisa, sijawahi kusikia mtu amefanya
hivyo bungeni ,” alisema Sara.
Mbunge wa Viti Maalum ( Chadema) ,
Chiku Abwao.
Kwa upande wa Mbunge wa Viti Maalum
(Chadema) , Grace Sindato Kiwelu , alisema :
“Sitegemei upande huo wa wabunge kupata
mimba zisizotarajiwa , kwani wanaofanya
mapenzi ni watu wazima hivyo wanafanya
wakijua kwamba wanatarajia kupata nini.”
Mbunge mwingine wa Viti Maalum
(Chadema) , Chiku Abwao , alisema: “Hakuna
mbunge anayepata mimba isiyotarajiwa,
kwanza nilimshangaa mbunge kutamka
mambo kama hayo, alistahili kuwaambia
watoto , lengo lake lilikuwa kudhalilisha
wanawake. ”
Mbunge wa Viti Maalum (CCM ), Munde
Tambwe, alisema: “ Ile kauli ya Lusinde
kwamba kuna wabunge wanapata mimba
zisizotarajiwa, nadhani kuna mtu alikuwa
anamlenga, kwa hiyo mimi siwezi
kulizungumzia.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads