YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Alhamisi, 16 Mei 2013

RIPOTI YA WIKI : MAYAI FEKI YASAMBAA DAR ES SALAAM

-Yanatoka nchi jirani , yatengenezwa
kwa umeme
Makala na Denis Mtima na Chande
Abdallah
Ripoti ya Wiki hii imegundua kuwa asilimia
kubwa ya mayai yanayotumiwa na
wananchi wengi kwa sasa ni feki na
yanauzwa kinyemela ndani ya Jiji la Dar.
Baada ya kupigwa vita na serikali miezi
michache iliyopita , imebainika kuwa bado
yamezagaa na watu wanaotajwa kuyatumia
kwa kiasi kikubwa ni wauza chipsi mitaani .
Mayai hayo ambayo hayatofautiani na
mayai ya kuku wa kizungu yaliyozoeleka
kwa kuwa na muonekano wa rangi nyeupe
sana, imebainika kuwa yanatengenezwa
kwa kutumia mashine maalum za umeme.
Ili kubaini uwepo wa mayai hayo ambayo
serikali kupitia Bodi ya Chakula na Dawa
(TFDA ), iliwatahadharisha wananchi
kutotumia kwa madai kuwa yana madhara
kiafya, cha kushangaza bado yamezagaa
mitaani kama njugu.
Ripoti ya Wiki imejaribu kufanya utafiti wa
kina na kugundua uwepo wa mayai hayo
hasa katika maeneo ya Buguruni na Sinza ,
Dar ambapo ilidaiwa kuwa mzigo mkubwa
wa mayai hayo ulitokea nchini Kenya.
Aidha, kuanza kuuzwa tena kwa mayai hayo
siku za hivi karibuni , kunatokana na wakazi
wa jiji kutojali aina ya vyakula
wanavyokula, jambo linalotoa mwanya kwa
wachuuzi hao kuyapenyeza mayai hayo kwa
siri kwenye mzunguko wa mayai ya
kawaida.
Ripoti ya Wiki ilizungumza na mmoja wa
wauza chipsi waliokutwa na mayai hayo
ambaye alikiri uwepo wa mayai hayo na
kubainisha kuwa yanasambazwa na wauzaji
wakubwa ambao wanasemekana kuwa
waliyanunua kwa wingi kabla serikali
haijayapiga marufuku .
“Haya mayai mbona yapo mengi tu. Sinza
nzima, ukiuliza unayapata. Watu wengi
wanayakataa. Ambao hawayajui
tunawabambikizia wanakula, ” alisema
muuza chipsi huyo kwa sharti la kutotajwa
jina

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads