WASOMI wanasema , ukisimamia vizuri kazi
uipendayo , itakupa faida kubwa na
kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. Lakini
unapohama fani hii mara umeacha hii na
kufanya nyingine , utakuwa mtu wa
kuyumba ( kigeugeu).
Snura Mushi .
Ulimwengu wa mastaa Bongo
umegawanyika katika vipengele
tofautitofauti, wapo wanaofanya filamu,
muziki, utangazaji na kadhalika .
Wapo walioweka nia tangu awali ,
wakasimama kidete na kuhakisha
wanafanikiwa katika kipaji walichoona
wapo sahihi na kweli miaka nenda rudi,
wakabaki katika fani husika wakiwa na
mafanikio.
KWA NINI WAHAME?
Kuna wengine walianza kama waigizaji ,
wakakomaa kwenye uigizaji lakini baadaye
wakabadilisha fani, sababu kubwa ikitajwa
kuwa ni kutafuta mlango mwingine wa
kutokea.
Sitaki niwaseme juu ya kuhama kwao
kwenye fani yao ya asili lakini wanapoicha
ni kama wameitelekeza au kuikimbia fani
husika na kujaribu nyingine , wanakosa
msimamo.
Miriam Jolwa ' Jini Kabula' .
JE, WANAFANIKIWA ?
Idadi kubwa ya mastaa ambao wameikacha
fani yao ya asili na kuhamia katika fani
nyingine huwa hawafanikiwi kwa asilimia
mia moja . Wengi wao huwa wanasuasua , ni
vyema wakajifunza kuwa na moyo wa
kukomaa.
Wafuatao ni baadhi ya wasanii ambao
walihama kutoka kwenye gemu la uigizaji
na kujitosa katika muziki wa Bongo Fleva .
Watazame mmoja baada ya mwingine;
ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE ’
Alianza vizuri katika soko la filamu ,
ametengeneza filamu kadhaa zikainga
mtaani . Tanzania ikapata kumjua kupitia
kivuli hicho cha filamu lakini baadaye
akaingia kwenye muziki wa Mduara .
Anajikongoja.
Zuwena Mohamed ' Shilole'.
SNURA MUSHI
Akiwa shosti wa Wema Sepetu enzi hizo,
watu wengi walimtambua kwa kuigiza .
Baada ya ushosti kuvunjika, Snura
alijiingiza kwenye gemu la muziki . Mambo
siyo mabaya anasumbua na wimbo wake
wa Majanga.
SALMA JABU ‘NISHA ’
Tupa kule kupambana katika staili ya
kutoka alikokupigania kwenye ‘industry ’ ya
filamu, amepambana lakini mwaka jana
akaona ajiingize katika gemu la muziki ,
wakatoa wimbo wa Sinaga , ulichezwa
kidogo lakini kwa sasa kimya.
JACQUELINE PENTZEL ‘ JACK CHUZ’
Huyu alianza kung ’ara katika Tamthiliya ya
Jumba la Dhahabu, baadaye kwenye filamu
lakini hatimaye akajitosa katika kundi la
muziki wa Bongo Fleva , Scorpion Girls .
Anasuasua .
MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’
Alianzia katika tamthilia, filamu na sasa
amejiunga na Kundi la Bongo Fleva ,
Scorpion Girls , mambo bado si mambo.
Hang ’ari kuliko alivyokuwa kwenye filamu .
Ukitazama utagundua idadi kubwa ya
waigizaji hao wanaohamia katika muziki
huwa hawafanyi vizuri sana. Mtazame
mwigizaji kama Flora Mvungi alipoingia
kwenye muziki , hakufanya vizuri kama
ilivyokuwa kwa Isabella Mpanda ambaye
alizitosa filamu kisha muziki ambao bado
haumlipi kiivyo.
Translate
Alhamisi, 16 Mei 2013
MASTAA HAWA WAMEIKIMBIA GEMU
About Young Concious
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni