Rais Jakaya Kikwete amemwagia sifa
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa
hatua ambayo inaweza kutafsiri mengi
katika medani ya siasa nchini.
Akizungumza na wabunge wa CCM
kwenye Ukumbi wa White House Dodoma
juzi, Rais Kikwete ambaye pia mwenyekiti
wa chama hicho, alisema nguvu za
Lowassa pekee zinatosha kushinda
uchaguzi mdogo wa kiti cha udiwani Kata
ya Makuyuni kilichoko wilayani Monduli.
Kata ya Makuyuni iko wilayani Monduli,
ambako Lowassa amekuwa mbunge wake
tangu mwaka 1995.
Habari za kutoka ndani ya kikao hicho
zinaeleza kuwa Rais Kikwete alitoa kauli
hiyo kuhusu kampeni za uchaguzi huo wa
Makuyuni, baada ya kuwa ametoa ruksa
kwa makada wa chama hicho wanaotaka
urais kuanza kujipitisha pitisha miongoni
mwa wanachama wa chama hicho.
Lowassa anatajwa kuwa miongoni mwa
wanaCCM wanaotaka kumrithi Rais
Kikwete kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka
2010.
“Sina tatizo na pale Makuyuni, najua
muscles (misuli) za Mzee Lowassa
zinatosha kutupa ushindi; au vipi mzee?”
alidokeza mmoja wa wabunge wa CCM
akimnukuu Rais Kikwete.
Uchaguzi wa Udiwani Kata ya Makuyuni
unaotarajiwa kufanyika Juni 16, mwaka
huu, utakuwa wa ushindani mkali kati ya
CCM na Chadema ambao historia yao
kisiasa mkoani Arusha ni ya uhasama.
Katika uchaguzi huo, unaofanyika baada
ya kifo cha Abdillah Warsama (CCM),
chama hicho kitatetea nafasi yake kwa
kumsimamisha Godluck Lerunya na
Chadema ni Japhet Sironga.
Mbali na Kata ya Makuyuni, uchaguzi wa
udiwani mkoani Arusha utafanyika pia
katika Kata za Kaloleni, Themi, Kimandolu
na Elerai, kutokana na waliokuwa
madiwani wa kata hizo (Chadema),
kufukuzwa na chama chao.
“Mnaweza kuchafuana leo, kesho mkapata
mgombea mwenye nundu nyingi na
mabandeji kila mahala, halafu mkapata
shida kumnadi,” alisema.
Siyo mara ya kwanza kwa Kikwete
kumsifia Lowassa kwani aliwahi kufanya
hivyo mwaka jana huko Longido wakati
akikabidhi ng’ombe.
Pia aliwahi kumsifia wakati wa kampeni
za uchaguzi za mwaka 2010 wakati
Kikwete alipomwelezea Lowassa kama
Mbunge makini na kuwaomba watu wa
Monduli kumchagua tena.
Hata hivyo, alipoulizwa kama baada ya
kuruhusiwa kuanza kujipitisha kwa
wanaCCM kama anataka kuwania urais,
Lowassa alijibu kupitia watu wake wa
karibuni kuwa asingependa kuzungumzia
suala hilo hasa baada ya Rais kutoa kauli
hiyo.
Kutangaza nia ruksa
Rais Kikwete aliwaeleza wabunge hao
kuwa si kosa kwa watu kutangaza nia ya
kugombea nafasi mbalimbali za uongozi
ikiwamo urais mwaka 2015.
“Wabunge na mawaziri wenye nia ya
kutangaza nia ya kugombea urais wawe
huru, kwani hiyo ni haki yao, isipokuwa
wafanye kwa wema bila kukivuruga chama
na kuwagawa wanaCCM katika makundi.
Sioni tatizo watu kujipitisha. Sisi sote
hapa tulijipitisha. Lakini tufanye hivyo
kistaarabu bila kuvurugana.”'
Aliwaagiza wabunge wa chama hicho
kwenda majimboni mwao kusikiliza kero
za wananchi badala ya kusubiri wakati wa
uchaguzi.
Kauli ya Membe
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Bernard Membe ambaye
naye anatajwa kuwa miongoni mwa
wagombea amewataka waandishi waache
kuandika kila siku habari za urais na
badala yake waandike mambo ya
maendeleo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana
baada ya kukutana na mabalozi wa nchi
zinazoendelea kuhusu Mkutano wa Smart
Partnership, unaotarajiwa kufanyika
nchini, Membe alisema ni vizuri
yakaandikwa mambo ya maendeleo na si
kila wakati kuandika mambo ya urais.
“Mkutano kama huu nchi kama Kenya
watauripoti vizuri na kwa undani hivyo
mfanye hivyo si kila kitu urais 2015,”
alisema Membe.
Mkutano huo utaanza Mei 28, hadi Juni
Mosi na utajadili jinsi gani sayansi na
teknolojia vinaweza kutumika
kuzikwamua kiuchumi.
CHANZO: MWANANCHI
Translate
Jumanne, 21 Mei 2013
RAIS KIKWETE AMWAGIA SIFA LOWASSA......AMEDAI KWAMBA LOWASSA NI "JEMBE"
About Young Concious
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni