MPANGILIO wa alama mpya za kufaulu
kwa wahitimu wa kidato cha sita
waliohitimu mwaka jana, ambao matokeo
ya mitihani yao yanaweza kutangazwa
wakati wowote kuanzia sasa, unadaiwa
kuzua aibu na kama si uamuzi uliotajwa
bungeni wa matumizi ya alama za ufaulu
za zamani, matokeo hayo yangeibua aibu
kama ilivyojitokeza kwa kidato cha nne,
2012.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari
kutoka Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA)
ambalo linaendelea kupanga matokeo hayo
ya kidato cha sita kwa kuzingatia alama za
zamani kama ambavyo taarifa ya awali ya
Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda, ilivyosomwa bungeni hivi
karibuni, hali ingekuwa mbaya zaidi
katika ufaulu kwa wanafunzi wa kidato
cha sita kiasi cha kuweza kutishia uhai wa
vyuo vikuu nchini kukosa wanafunzi wa
kutosha.
“Hali ilikuwa mbaya sana kama alama za
kufaulu zingeachwa zitumike zile mpya
na si za zamani. Vyuo vikuu nchini
visingeweza kupata wanafunzi wa
kutosha.
"Tatizo hapa si uwezo wa wanafunzi moja
kwa moja katika kumudu mitihani bali ni
kufanywa kwa mabadiliko ya alama bila
kuwaandaa.
" Alama hizi zilipaswa kuanza kutumika
na wanafunzi wapya, yaani kama
wanaanza kidato cha kwanza wawe
wanapewa mitihani ya kupimwa kwa
kuzingatia alama mpya na waendelee nazo
hadi mitihano yao ya mwisho.
“Na hivyo hivyo kwa wanafunzi wa kidato
cha sita. Alama hizi mpya zinapaswa
kutumika kwako kuanzia wakiwa kidato
cha tano mara wanapoanza shule, kila
mitihani wanayopewa isahihishwe na
kupangiwa alama kwa kutumia hizi alama
mpya,” kinaeleza chanzo chetu cha habari
kutoka NECTA.
Kwa mujibu wa mabadiliko hayo ya
alama, alama mpya zilizokuwa
zimetumika awali ni daraja F kuanzia 34
hadi sifuri; badala ya alama hiyo F
kuanzia 20 hadi 0; daraja D kwa
kuzingatia alama mpya linapaswa kuanzia
35 tofauti na awali, yaani alama 21.
Taarifa zaidi zinabainisha ya kuwa, kati
ya sababu za kuchelewa kutangazwa kwa
matokeo ya kidato cha sita tofauti na
muda uliotarajiwa yaani mwanzoni mwa
Mei, ni pamoja na upangaji upya matokeo
hayo, ikiwa ni tofauti na ilivyokuwa kwa
kidato cha nne ambapo matokeo
yalitangazwa na kisha kufutwa ili
kuyapanga upya kwa kutumia alama za
zamani.
Lakini alipoulizwa kuhusu masuala hayo
ndani ya NECTA, Ofisa Habari wa Taasisi
hiyo nyeti nchini, John Nchimbi alisema;
“Kwa sasa niseme tu kwamba mchakato wa
kuandaa matokeo ya kidato cha sita
unaendelea, siwezi kusema lini hasa
utakamilika lakini nina uhakika ni katika
muda muafaka.”
Kuhusu matokeo ya kidato cha sita
kucheleweshwa kutokana kupangwa upya
ili kupunguza idadi ya waliofeli kutokana
na matumizi ya alama mpya za kufaulu,
Nchimbi anasema; “Unajua haya maagizo
haya ya bungeni (kupanga matokeo kwa
kuzingatia alama za zamani) yamekuja
wakati mchakato wa kuandaa matokeo
ulikwishaanza. Kwa hiyo baada ya
maagizo ilibidi kufanya kazi hiyo tena kwa
kufuata maagizo hayo.”
Hata hivyo, hakuweka bayana kama
matokeo ya awali kabla ya maagizo ya
Serikali yaliyotolewa bungeni kutumia
alama za zamani yamewafanya wanafunzi
wengi kufeli na badala yake akasema;
“Hilo siwezi kulizungumzia kwa sababu
mchakato wa matokeo hayo haukuwa
umefika mwisho. Takwimu rasmi
hazikuwa zimekamilishwa. Kwa hiyo si
sahihi kusema rasmi walifeli.”
Lakini wakati hali ikiwa hivyo kwa
upande wa matokeo yanayotarajiwa ya
kidato cha sita, taarifa zaidi zinabainisha
ya kuwa, baada agizo la serikali la kufuta
na kurejewa upya kwa matokeo ya kidato
cha nne mwaka 2012, takriban wanafunzi
50,000 wamepata unafuu katika matokeo
yao tofauti na awali.
Awali, kwa kuzingatia matokeo ya kidato
cha nne mwaka jana yaliyotangazwa
Februari, mwaka huu jijini Dar es Salaam,
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dk. Shukuru Kawambwa, jumla ya
watahiniwa 126,847 tu kati ya watahiniwa
397,136 waliofanya mtihani huo
walifaulu.
Katika matokeo hayo idadi ya wasichana
waliofaulu ilitajwa kuwa ni 46,181 wakati
wavulana waliofaulu ikiwa wanafunzi
80,686 na idadi ya watahiniwa wa
kujitegemea waliofaulu ni 16,112 kati yao
watahiniwa 61,001 waliofanya mtihani
wasichana ni 6,7751 na wavulana 9,361.
Katika matokeo hayo watahiniwa
waliopata daraja la kwanza ni 1,641,
daraja la pili 6,453 na daraja la tatu ni
15,426, wakati waliopata sifuri ni 240,903
lakini kwa kuzingatia taarifa za vyanzo
vyetu ndani ya Baraza, idadi hiyo
itabadilika kwa sababu ya alama
kuongezwa kwa watahiniwa hao wa
mwaka 2012.
Lakini matokeo hayo yalitangazwa pamoja
na vituko walivyofanya baadhi ya
wanafunzi, vikiwamo vituko vya kuandika
matusi kwenye karatasi za majibu ya
mitihani na kutokana na makosa hayo,
watahiniwa 789 walifutiwa mitihiani yao.
Source: Raia Mwema.
Translate
Jumanne, 21 Mei 2013
" MATOKEO YA KIDATO CHA SITA".....SIFURI KIBAO ZAFUTWA KIMYA KIMYA
About Young Concious
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni