MREMBO aliyepata umaarufu kupitia
Shindano la Maisha Plus Season II ,
Jacqueline Dustan ‘ Jack’ amepata ajali
mbaya ya gari maeneo ya Msamvu mkoani
Morogoro na kupata majeraha usoni na
mguuni.
Akizungumza na Exclusive Star, Jack
alisema Jumanne iliyopita walikuwa kwenye
teksi yeye na marafiki zake wengine
wakielekea maeneo ya Kihondo mkoani
humo kumsalimia mjomba wake ndipo
walipogongana na gari lingine katika
‘round about’ ya Msamvu na
kumsababishia majeraha hayo .
Mara baada ya kupata ajali hiyo, Jack
alisema alikimbizwa katika Hospitali ya
Maria mkoani humo ambapo alipata
huduma ya kwanza na sasa anaendelea
vizuri.
“Namshukuru Mungu naendelea vizuri ,
angalau sasa naweza hata kutoka nje
tofauti na mwanzo nilivyokuwa ,” alisema
Jack.
Translate
Jumamosi, 25 Mei 2013
MASIKINI!!JACK DUSTAN APATA AJALI YA GARI.:HABARI KAMILI soma hapa
About Young Concious
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni