Mheshimiwa huyo alimudu kuwafanya
waheshimiwa wacheke sana huku ujumbe
ukifika tofauti na mawaziri wengine waliopita
ambao hotuba zao zinadaiwa kuwa zilijaa
ushawishi wa usingizi.
“Tunajenga barabara kwa kiwango cha lami
kutoka Dodoma kwenda Iringa, wale watani
zangu wa Iringa hawatakuwa na haja ya
kujinyonga kwenye miti, sasa watakuwa
wakilala barabarani tu.”
Wabunge walivunjika mbavu kwa vicheko.
Watani zake alimaanisha Wahehe ambao
inadaiwa wanapokuwa na hasira wana tabia ya
kujiua kwa kujinyonga (ni madai).
Kama vile haitoshi, waziri huyo akijibu swali la
Mbunge wa Same Mashariki, Mheshimiwa
Anne Kilango Malecela kuhusu barabara
inayopita kwenye Kiwanda cha Tangawizi
kupewa hadhi, pia alitumbukiza utani.
“Mheshimiwa Anne Kilango yale uliyosema
tunayafanyia kazi, kuhusu barabara inayopita
Kiwanda cha Tangawizi kupewa hadhi
tumepokea, maana pia mheshimiwa rais
alitupa maagizo.
“Nimeamini una akili sana ndiyo maana mtani
wangu Malecela alitoka Dodoma na kwenda
milimani Same huko, kwa nini hakuja
usukumani?”
Aidha, waziri huyo akimjibu Mbunge wa
Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ambaye
alitoa ushauri kwa Wizara ya Ujenzi kupunguza
idadi ya miradi na kukamilisha mmoja baada
ya mwingine ili wizara iweze kufanikiwa huku
akilalamikia kutojengewa barabara jimboni
kwake, Magufuli aliwavunja mbavu tena
wabunge:
“…ushauri wako ni mzuri ndiyo maana wizara
yangu imeamua kuacha kujenga barabara
jimboni kwako ili tukamilishe sehemu nyingine
kwanza…”
Hata hivyo, wakati wabunge wakivunjika
mbavu, Magufuli alisema Serikali ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) haina ubaguzi na
itajenga barabara hiyo iliyoko jimboni kwa
mbunge huyo.
Akimjibu Mbunge wa Viti Maalum (CCM –
Bunda), Ester Bulaya ambaye alisema kwamba
anamkubali waziri huyo kutokana na utendaji
wake, Magufuli naye alisimama na kusema:
“Hata mimi namkubali Ester Bulaya...”
Aidha, Magufuli aliwashangaa wabunge wa
upinzani ambao walionesha kutaka kumpinga
na kuwaambia kuwa bosi wao, Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe alionesha
kumkubali na kuzimwagia sifa sera za CCM
baada ya kukamilishiwa barabara iliyoko
jimboni kwake Hai, Kilimanjaro.
“Kama kuna mtu anabisha ushahidi uko hapa
aje nimuoneshe, mheshimiwa aliandika kwenye
mtandao (akautaja jina zima) kisha akasema
kama mtu haamini akatoa flashi yenye sauti
aliyodai ni ya Mbowe.
VIDOKEZO VINGINE:
Alimwambia mbunge wa upinzani ana moyo
wa CCM CCM, amekaa ki-CCMCCM.
Katika kutekeleza uvunjaji wa nyumba
zilizoingilia hifadhi ya barabara aliwahi
kuvunja ukuta wa nyumba ya baba yake mzazi.
Translate
Jumamosi, 18 Mei 2013
Home
/
Unlabelled
/
MAGUFURI AGEUKA JOTI
BUNGENI, HIVI NI BAADHI YA
VICHEKESHO ALIVYOTOA
BUNGENI. SOMA HAPA
MAGUFURI AGEUKA JOTI BUNGENI, HIVI NI BAADHI YA VICHEKESHO ALIVYOTOA BUNGENI. SOMA HAPA
About Young Concious
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni