KAULI ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi
(CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, kwamba
kuna njama za kumwongezea Rais Jakaya
Kikwete, muda wa kuongoza nchi, ni uzushi
mtupu na ni upotoshaji usiokuwa na msingi.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu
iliyotumwa kwa vyombo vya habari juzi,
ilifafanua kwamba Rais Kikwete hafahamu
kuwepo mipango hiyo, na kumtaka Profesa
Lipumba aisaidie jamii kusema nani anafanya
mpango huo, ili ukweli ujulikane.
“Aidha, Mheshimiwa Rais anawasihi wanasiasa
na Watanzania kwa ujumla, kuacha tabia za
uongo na uzushi na kuwapotezea muda
Watanzania kufikiria mambo yasiyokuwepo.
“Ukweli ni kwamba, kama ambavyo amesema
mara nyingi, ni matarajio ya Rais Kikwete
kuwa mchakato wa Katiba utakamilika mwaka
2014, na kuwezesha Uchaguzi Mkuu wa 2015
kufanyika chini ya Katiba Mpya kama
inavyotarajiwa ,” ilieleza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa Ikulu, Rais Kikwete anatarajia
baada ya uchaguzi wa 2015, atapata nafasi ya
kustaafu mwisho wa kipindi chake cha uongozi
kwa taifa letu.
Translate
Jumamosi, 18 Mei 2013
Home
/
Unlabelled
/
HII NDO KAULI YA IKULU KUA
LIPUMBA NI MUONGO NA
MZUSHI, SOMA HAPA KUJUA
CHANZO NI NINI
HII NDO KAULI YA IKULU KUA LIPUMBA NI MUONGO NA MZUSHI, SOMA HAPA KUJUA CHANZO NI NINI
About Young Concious
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni