BINTI mrembo aitwaye Flora Bahati Lyimo
anamtuhumu mbunge mmoja wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
linaloongozwa na Spika Anne Makinda
kuwa amembaka ...
Katika uchunguzi wake, hivi
karibuni ,Uwazi lilielezwa kuwa kuna
habari ya kashfa nzito inayomtafuna
mbunge huyo anayetokea Kanda ya
Kaskazini lakini haikufafanua kwamba
inahusu nini.
Baada ya kutulia na kupekua kwenye
vyanzo vyake, Uwazi lilibaini kuwa kashfa
inayomlenga mheshimiwa huyo ni ya
ubakaji na tayari imefikishwa
mahakamani huko London nchini
Uingereza.
Habari hiyo ilielezwa ‘kijuujuu’ hivyo
uwazi likamtafuta Flora ambaye ni
Mtanzania anayetokea mkoani Kilimanjaro
ambaye anaishi katika Jiji la London
kikazi.
Alipopatikana Flora alibanwa kisawasawa
ndipo akaibua mazito huku akieleza tukio
zima lilivyofanyika kwa data na vielelezo
vya kila aina ikiwemo barua ya
Mahakama ya Crown ya London.
“Ni kweli mheshimiwa … (anamtaja jina)
alinibaka Agosti, mwaka jana. Yeye na
makada wenzake wa chama chake
walikuja hapa London kwa ziara ya
kichama na kwa kuwa mimi sina chama
nilikwenda kuhudhuria mkutano wao kwa
kuwa nina mtandao wangu (blog) hivyo
nilitaka kupata habari za kuingiza kwa
sababu ni za watu wa nyumbani
(Tanzania).
Akiendelea kuweka wazi kisa hicho, Flora
anasema: “Nikiwa kwenye mkutano….(jina
la mbunge) alinifuata akaniuliza
nimeandika watu wangapi waliohudhuria
mkutano huo, nikamjibu 50 akaniambia
niongeze idadi hiyo ili ionekane mkutano
ulikuwa na watu (Watanzania waishio
Uingereza) wengi.
“Hapo ndipo alipoanza kunizoea. Alitaka
kunipa kadi ya chama chake nikakataa,
ndipo akadai kwamba mimi nilitumwa
kwenye mkutano huo na balozi na rais
kwa ajili ya ushushushu.
“Mkutano ulimalizika, sasa nilipokuwa
naondoka kurudi nyumbani kwangu,
mbunge huyo na wenzake nao walitoka.
Tukiwa njiani wenzake walikwenda
kujisaidia haja ndogo, yeye akaniomba
akajisaide nyumbani kwangu,
nilimkubalia.
Alipofika ndani, bila kujua kila kitu
kinaonekana kwenye kamera alinibadilikia
kama vile adui vitani, ona sasa wema
wangu ukawa umeniponza.
Alinirukia, akaniburuza hadi kitandani
kwangu. Nilipokuwa mkali na kwa namna
nilivyokuwa nimechanganyikiwa sishikiki
ndipo akanivamia maungoni, akanichania
nguo zangu akitaka nimwachie atimize
lengo lake la kuniingilia kimwili kwa
nguvu.
“Nilijitahidi ili asifanikiwe, nikamwambia
amekwisha kwani lazima nimwanike
ndipo akanipiga nusu aniue akisisitiza
kuwa kama nitauanika uovu wake huo au
kuchukua hatua zozote ataniua.
“Inaniuma sana, kunibaka anibake halafu
atishie kuniua, unyama gani huu?”
Flora anaendelea kusema:
“Katika purukushani hiyo, nilipopata
mwanya kidogo tu, nikapiga namba ya
polisi 999 kuomba msaada. Alipoona hivyo
alitoka na kutokomea kusikojulikana.
Polisi walipofika hawakufanikiwa
kumkamata.”
Flora alisema polisi walimchukua na kila
kitu cha ushahidi zikiwemo nguo zake hadi
kituoni, wakamhoji kwa kumrekodi sauti,
wakampa namba ya jalada la kesi
inayosomeka; 4621279/2012-UBAKAJI/
KUTISHIA KUUA ambapo hadi leo mbunge
huyo anasakwa na Polisi wa London,
akikanyaga tu Uingereza lazima akamatwe
akajibu tuhuma za ubakaji na kutishia
kuua.
Flora akaongeza: “Ukweli ni kwamba
hakufanikiwa kukamatwa kwa sababu
alikuwa na passport za kidiplomasia
ambazo nyingine hakutumia jina lake
halisi.
“Kesho yake nilisikia alikimbilia
Ujerumani, nikawaambia polisi lakini
walikumbana na tatizo lile kwani majina
niliyowapa siyo aliyotumia kuingia Ulaya.
“Januari mwaka huu nilipotaka kurudi
nyumbani Kilimanjaro, mahakama ya
hapa (Uingereza) ilinipa barua ambayo
nilipofika niliipeleka Kituo Kikuu cha
Polisi Moshi nikafunguliwa faili Namba
Mos/RB/17127/12 kwa ajili ya ulinzi chini
ya R.C.O Ramadhan Ng’anza.
“Niliwaeleza kuwa mtu anayetaka kuniua
ni mbunge huyo. Kweli waliahidi
kunisaidia, nilipoondoka kurudi London
niliwasiliana na polisi Kilimanjaro lakini
niliona kama kuna kitu au mbunge huyo
yupo juu ya sheria kwani walikana
kunifahamu.
“Sitachoka kutafuta haki na kutetea
wanawake wanaobakwa kila siku wanaona
aibu kusema, naamini aibu haipo kwa
mbakwaji bali kwa mbakaji, yule ….
(anataka jina) ni mbakaji.
“Nimesharipoti mashirika mengi ya haki
za binadamu ya Uingereza. Kuna siku
nilishinda mahakamani, kule ni yeye tu
anasubiriwa atiwe mbaroni akasimame
kizimbani ndipo dunia itajua
ninachokisema.”
Flora allisema kama kweli mbunge huyo ni
mwanaume aende tena jijini London kama
hatasimamishwa kizimbani na kuozea
jela.”
Chanzo: Gazeti la uwazi
Translate
Jumanne, 14 Mei 2013
FLORA BAHATI LYMO NI MWANAMKE ANAYEDAI KUBAKWA NA MBUNGE WA TANZANIA
About Young Concious
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni