YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Ijumaa, 31 Mei 2013

DIAMOND: JOKATE NISAMEHE ===>>bofya hapa kupata habari

MKALI wa Bongo Fleva , Nasibu Abdul
‘Diamond’, ameibuka na kuelezea kuhusu
uhusiano wake na mpenzi wake zilipendwa,
Jokate Mwegelo ‘Kidoti ’ ambaye ni
mwigizaji na modo moto wa kuotea mbali
Tanzania .
Nasibu Abdul ‘Diamond ’ akiwa na Jokate
Mwegelo ‘Kidoti ’.
Akizungumza kwa uhakika kabisa, Diamond
alisema inampasa amuombe radhi Jokate
kwa sababu katika uhusiano wao, Jokate
hakuwahi kumkosea ila yeye ndiye tatizo
na chanzo cha kuachana kwao .
Diamond alisema hayo kwenye mahojiano
na Mtangazaji Zamaradi Mketema katika
Runinga ya Clouds kwenye Kipindi cha Take
One, kilichorushwa juzi Jumanne usiku
kituoni hapo .
DIAMOND ANAFAFANUA
“Inanipasa nimuombe radhi Jokate. Ni
kweli nilimtenda vibaya wakati wa mapenzi
yetu. Hakukosea sana maana hakuwahi
kufanya jambo lolote kinyume . Sijui
niseme nini lakini nataka kueleza wazi
kuwa mimi ndiyo sababu ya kuachana
kwetu na ilitokea tu.
Image
.. .Diamond na Jokate wakicheza .
“Naamini hilo jambo lilimuuma sana ,
maana nakumbuka wakati ule , baada ya
mimi kurudi kwa Wema (Sepetu ), watu
walimwandama sana kwa maneno na
alionekana msaliti lakini ukweli ni kwamba
nilimpenda sana lakini ndiyo hivyo , siwezi
kufafanua zaidi.
“Kutoka moyoni mwangu , namuomba
msamaha Jokate , kama hatanisamehe
nitaendelea kumuomba mpaka naingia
kaburini. Sina raha kabisa kutokana na
jambo hilo. Lazima niwe mkweli.”
JACQUELINE WOLPER
Diamond alikwenda mbali zaidi na
kuwazungumzia baadhi ya wasichana
aliowahi kutoka nao kimapenzi akiwemo
mwigizaji Jacqueline Wolper ambaye
alisema ni mwanamke aliyempenda sana ,
ndiyo maana alimtungia wimbo wa
Mawazo.
PENNY SASA
Kwa upande wa mpenzi aliye naye sasa,
Mtangazaji wa Runinga ya DTV, Penieli
Mungilwa ‘ Penny’ alisema ni mwanamke
mtulivu na sahihi kwake kwa sababu
anatambua majukumu yake kwake, pia
anamheshimu .
“Huyu kwa kweli ana karibu sifa zote
alizonazo Wema ila uzuri wa Penny
ananiheshimu sana . Hafanyi mambo yake
hadharani. Unajua wakati nikiwa na Wema
hata kama akifanya mambo yake siku mbili
au tatu baadaye nayaona kwenye magazeti,
tofauti na Penny ambaye kwangu mimi
naona ananiheshimu , hata kama anafanya
mambo yake ni kwa siri . ”

SOURCE: www.globalpublishers.info/m/blogpost?id=5398006%3ABlogPost%3A2024504

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads