YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumatatu, 20 Mei 2013

BINTI ATOROKEA UINGEREZA AKIKWEPA KUTOMASWA NA MFALME MSWATI

Msichana mdogo ameomba hifadhi ya
ukimbizi nchini Uingereza baada ya
kukataa kwa dharau harakati za ndoa za
wake wengi za Mfalme Mswati III wa
Swaziland na kugoma kujiunga kwenye
nyumba harimu ya wake 13.
Tintswalo Ngobeni, mwenye umri wa
miaka 22, alitimkia Uingereza kutoka taifa
hilo la kusini mwa Afrika akiwa na umri
wa chini ya miaka 18 baada ya kuvuta
hisia za mfalme huyo milionea, mtawala
maarufu mkandamizaji kwa maisha yake
ya anasa.
Ikiwa ni sehemu ya mila za Swazi, Mfalme
Mswati III, mwenye umri wa miaka 45,
anaruhusiwa kuchagua mke mpya kila
mwaka.
Tintswalo, ambaye sasa anaishi mjini
Birmingham, alikuwa na umri wa miaka
15 tu wakati Mfalme huyo alipofanya
harakati zake baada kumuona kwenye
jumba la kifalme la mke wake wa nne,
LaNgangaza. Binti huyo alisema 'alitishika'
pale alipogundua dhamira zake za ndoa.
Aliongeza: "Alianza kunipigia simu
kwenye shule ya bweni. Aliniuliza kama
ningetaka kuwa sehemu ya familia ya
kifalme. Ilinibidi kukaa kimya kuhusu
mashaka yangu lakini nilifahamu
sikutaka kuolewa naye na kujitolea
maisha yangu kwa mfalme huyo.
"Wake zake wamewekwa kwenye
majumba yao, wakizingirwa na walinzi,
na hakika hawawezi kwenda kokote
isipokuwa tu mfalme akisema hivyo. Kitu
pekee wanachofanya ni kwenda Marekani
mara moja kwa mwaka, wakati mfalme
huyo anapowapatia posho kwa ajili ya
manunuzi."
Tintswalo alikuwa amelazimishwa
kuachana na maisha ya starehe kwenye
shule moja ya bweni huku shangazi yake,
ambaye alikuwa mlezi wake mkuu,
akisuka mipango ya kutorokea Uingereza
kuungana na mama yake, ambaye
alihamia mjini Birmingham miaka mitano
kabla, akimtoroka mume wake
mnyanyasaji.
"Sikuwa na jinsi," alisema. "Hakuna
aliyewahi kumwangusha mfalme huyo au
kuthubutu kumdharau, hivyo nikatoweka
tu."
Tangu kuwasili nchini Uingereza,
Tintswalo amekuwa sauti ya upinzani
dhidi ya utawala kandamizi za Swazi,
ambapo vyama vya upinzani vya siasa
vimefungiwa na wanaharakati wamekuwa
wakikamatwa mara kwa mara au
kushambuliwa.
Hatahivyo, shughuli kuu za Tintswalo,
ikiwamo maandamano ya kila wiki nje ya
ubalozi wa Swazi mjini London akiwa na
kikundi cha Swazi Vigil, zimesikika kwa
mamlaka hizo nchini kwake na sasa
anaamini yuko kwenye hatari kubwa zaidi
kuliko ilivyowahi kutokea.
Alisema: "Hivi karibuni nilipata taarifa
kwamba watu wametumwa kutoka
Swaziland kuja kunikamata, jambo
ambalo hakika linanitisha mno. Kama
nikirejea, nitakamatwa au mbaya zaidi
huku pale kuna watu ambao wanateseka,
kupigwa au kuuawa kwa kujihusisha na
siasa."
Tintswalo sasa anaishi katika mashaka ya
kuweza kurejea nchini Swaziland, baada
ya ombi lake la kwanza la hifadhi ya
kisiasa nchini Uingereza mwaka 2007
kukataliwa mwaka 2011.
Mwezi uliopita, alikamatwa na kupelekwa
kwenye kituo cha kushikilia wahamiaji
baada ya miezi 18 ya kuripoti kila wiki
katika mamlaka hizo.
Hatahivyo, baada ya shinikizo kutoka TUC
na ofisi ya Mbunge wa Birmingham
kupitia chama cha Labour, Roger Godsiff,
Tintswalo aliachiwa na sasa amekata rufaa
wizara ya Mambo ya Ndani.
Godsiff alisema juzi: "Tumefurahishwa
mno wanasheria walifanikiwa sana katika
kuwezesha kutazamwa upya kwa kesi ya
Ngobeni."
Baba huyo wa watoto 27, Mfalme Mswati
III alikuwa mgeni kwenye harusi ya
William na Kate na pia kwenye sherehe za
Miaka 50 ya Malkia wakati wa majira ya
joto mwaka jana.
Mke wa sita wa mfalme huyo alitoroka
kutoka kwenye jumba hilo harimu mwaka
jana, akielezea miaka kadhaa ya
'machungu na udhalilishaji wa kimwili'
uliofanywa na mume wake.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani
alikataa kuzungumzia chochote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads