Dar na Dodoma. Wakati Spika wa
Bunge, Anne Makinda akitangaza
kuanza kuwatoa nje ya Ukumbi wa
Bunge wanaotumia lugha za matusi,
baadhi ya wanasiasa, wanaharakati na
wanazuoni wamesema wabunge
wanatumia mamilioni ya kodi za
wananchi, hivyo wanatakiwa
kuheshimu hilo na kujikita zaidi
kuzungumzia masuala ya msingi.
Juzi Mbunge wa Kondoa Kusini (CCM),
Juma Nkamia na Mbunge wa Mtera
(CCM), Livingstone Lusinde aliwapiga
vijembe viongozi wakuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
wakisema kwamba kuna wabunge
ambao wana “mimba zisizotarajiwa
bungeni.”
Kutokana na hali hiyo, Mbunge wa Viti
Maalumu (Chadema), Paulina Gekul
akitumia Kanuni ya 68 (7), alikilaumu
kiti cha Spika kwa kukaa kimya wakati
wabunge hao wanatukana bungeni.
Pia Moses Machali (Kasulu Mjini-
NCCR-Mageuzi) na Magdalena Sakaya
(Viti Maalumu-CUF) waliomba
mwongozo wa Spika wakitumia Kanuni
ya 64 inayozuia lugha za kuudhi
bungeni.
Wakizungumza jana kwa nyakati
tofauti Profesa Simon Mbilinyi
alisema, “Wabunge hawa wanatumia
vibaya fedha za walipakodi ambao
wanaishi maisha duni,
hawakuchaguliwa kwa ajili ya
kupigana vijembe bungeni.”
Mwenyekiti wa Kituo cha Sheria na
Haki za Binadamu (LHRC), Helen-Kijo
Bisimba alisema, “Inaonekana hawajui
cha kufanya wala kilichowapeleka
bungeni.”
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha
Walimu Tanzania (CWT), Ezekiel
Oluoch alisema kuwa moja ya mambo
yaliyotakiwa kujadiliwa na wabunge
hao ni pamoja na madai ya walimu ya
muda mrefu.
“Walimu wanaidai Serikali Sh25
bilioni, kuna suala la kutokuwapo kwa
mitalaa, haya yote hawayaoni
wanaishia kutupiana vijembe tu,”
alisema Oluoch.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha
Madaktari Nchini (MAT), Dk Rodrick
Kabangila alisema tatizo siyo wabunge,
bali ni Spika, Makinda.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe,
Profesa Prosper Ngowi alisema
wabunge wanatakiwa kutambua kuwa
wapo bungeni kwa fedha za wananchi,
hivyo wanatakiwa kulipa fadhila.
“Wananchi wanawategemea wabunge
wasimamie haki na usawa na kujenga
hoja za kutetea masilahi yao,naona
2015 ndiyo uwe muda wa wananchi
kuchagua anayewafaa ,” alisema
Profesa Ngowi.
Makinda kuwaitia polisi
Translate
Jumatano, 17 Aprili 2013
Matusi bungeni: wadau walaani wabunge
About Young Concious
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni