YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumatano, 17 Aprili 2013

Bilal awataka wadau sekta ya maji, umeme barabara kudhibiti utoaji huduma

Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Ghalib
Bilal akiwa na Mkurugenzi wa Ewura
Haruna Masebu wakati wa mkutano
Arusha

Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Ghalib
Bilal amewataka wadau wa sekta ya maji,
umeme, bara bara na usafiri katika nchi za
bara la Afrika kudhibiti njia za utoaji wa
huduma pamoja na kuwa wawazi bila
kufanya kazi kwa kuwa na ushawishi toka
katika sehemu nyingine.
Makamu wa Rais ametoa agizo hilo Jijini
Arusha wakati akifungua mkutano wa kumi
wa wadau 180 wa vyombo vya
miundombinu vya kiuchumi toka katika
nchi mbali mbali za Barara la Afrika,
ambapo amesema vyombo hivyo
vimewekewa utaratibu wa sera ya
kudhibiti ili viweze kufanyakazi vizuri.
Wadau wa masuala ya
maji,umeme,barabara na usafiri  toka
katika bara la Afrika wanakutana jijini
Arusha kwakushirikiana na Mamlaka ya
udhibiti wa Huduma  za Nishati na Maji-
EWURA- pamoja na Mamlaka ya udhibiti
wa nchi kavu na majini SUMATRA ,kujadili
changamoto mbalimbali zinazozikabili
sekta hizo huku kitu kikubwa ni namna
gani wataweza kuwa wawazi zaidi.
Kufuatia changamoto hiyo, Makamu wa
Rais Dkt. Bilal amesema ni vema wadau
wa sekta hizo wakawa wawazi zaidi ili
kubaini kitu gani kinachobainika ili kuweza
kuboresha zaidi sekta hizo ili kuweza
kutoa huduma nzuri.
Pia amesisitiza kuwa na chombo cha
kudhibiti katika sekta hizo ili kuweza kuwa
waadilifu zaidi katika kutoa huduma.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa
EWURA- ambaye pia ni Mwenyekiti wa
mkutano huo wa wadau, Haruna Masebu
amesema suala la uwazi katika kutoa
huduma za udhibiti ni zuri kwani
linaondoa vishawishi vya rushwa.
Pia Makamu wa Rais alizindua kitabu cha
udhibiti wa huduma za kiuchumi
kilichoandaliwa na Prof . Mark Mwandyosa
ambaye amesema ameamua kuandika
kitabu kwa ajili yakuweka mambo wazi
kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads