YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumatano, 17 Aprili 2013

Pinda, Mbowe ngoma nzito bungeni

Dar/Dodoma. Mvutano kuhusiana na
mchakato wa kupata Katiba Mpya
unaozigonganisha Serikali na Chadema
ulizidi kupamba moto bungeni jana
wakati wa mjadala wa kuhitimisha
hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri
Mkuu.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana
alitumia muda wake karibu wote wa
saa moja kujibu maoni na
kumshambulia Kiongozi wa Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman
Mbowe aliyoyatoa kuhusu hotuba ya
bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Hoja za Mbowe zilizoonekana
kumsumbua Pinda ni malalamiko dhidi
ya Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kauli
yake kwamba serikalini hakuna weledi
wa kuwezesha kupanga mipango ya
maendeleo.
Hata hivyo, baada ya kuhitimisha
hotuba hiyo, Mbunge wa Ubungo, John
Mnyika alisimama kuomba mwongozo
wa Spika chini ya kanuni ya 68 (7)
akidai kuwa Pinda alikuwa ametoa
kauli ya uongo kuwa Chadema
haikuwasilisha mapendekezo yake juu
ya muundo wa Mabaraza ya Katiba,
badala yake walilalamika tu kwenye
mkutano wa hadhara.
Akizungumzia, Pinda alieleza
kumshangaa Mbowe kwa kudai kuwa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba haina
weledi wakati kuna maprofesa na kati
ya hao ni Profesa Mwesiga Baregu wa
Chadema.
“Hivi kweli hawa wazee na maprofesa
ni mambumbumbu kweli au ni kauli
ambayo hakuipangilia. Haiwezekani
kwa mjumuiko wa wazee wote
waliomo mle ndani."
“Tuwatendee haki Watanzania na
tusiwakatishe tamaa wazee wetu
ambao wamezunguka nchi nzima na
kufanya kazi kubwa, kama haya ndiyo
Mbowe ametumwa basi nadhani
aliteleza.”
Pinda alisema kama kuna tatizo
kwenye mchakato ni kutokana na
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba
iliyopitishwa na Bunge.
Wakati anazungumzia suala hilo
ilisikika sauti kuwa wakati sheria hiyo
inapitishwa Chadema walitoka
bungeni, na Pinda alirudia, “Nasikia
kuwa mlitoka bungeni.”
Pinda alisema kutakuwa na Bunge la
Katiba na wabunge wote ni wajumbe,
pia kwa Zanzibar kuna Baraza la
Wawakilishi, hivyo Mbowe kuanza
kutoa maoni hayo inaonyesha wana
hofu.
“Kama Chadema wana hofu basi ni
jambo lingine, nilipoisoma
`speech’ (hotuba) ya Mbowe mawazo
yake yanaonyesha anawaza uchaguzi
wa 2015 na si kitu kingine,” alisema
Pinda na kupigiwa makofi na wabunge
wa CCM.
Alisema Mbowe alimtisha zaidi pale
aliposema kuwa wataitisha
maandamano nchi nzima kupinga
suala hilo, kitu ambacho si sawa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads