Utajiri wa
mwanamuziki Jay Z ulipanda kwa asilimia 30 mwaka jana na kufikisha
utajiri wake hadi $810m (£626m), kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Lakini
kuimarika kwa utajiri wake hakukutosha kumuondoa Sean "Diddy" Combs
kutoka kwenye kilele cha wanamuziki matajiri zaidi wa Hip Hop kwa mujibu
wa jarida hilo.Diddy anaongoza akiwa na utajiri wa jumla ya $820m (£633m).
Forbes walisema utajiri wake ulioimarishwa na mikataba ya kibiashara ambayo alitia saini na Diageo kwa ajili ya Ciroc vodka na mavazi yake ya Sean John.
Lakini rapa na produsa Jay Z alipanda hadi nafasi ya pili sana kutokana na uwekezaji wake wa $200m (£155m) katika kampuni ya kuuza muziki mtandaoni ya Tidal.
Pia, ana mvinyo kwa jina Armand de Brignac, na anamiliki pia Roc Nation.
Mwaka uliopita, utajiri wa Diddy ulikuwa $750m (£579m) na wa Jay Z $610m (£471m).
Forbes waliandaa orodha yao wakizingatia mapato ya miaka ya nyuma pamoja na stakabadhi za kifedha, thamani ya mali inayomilikiwa na wanamuziki hao na pia kwa kuzungumza na wachanganuzi, mawakili, mameneja na wataalamu wengine katika tasnia ya muziki.
Rapa wa zamani wa NWA Dr Dre kwa sasa ana utajiri wa $740m (£571m) baada ya kuuza Beats kwa Apple mwaka 2014 kwa $3bn (£2.3bn), lakini amepitwa na Jay Z kwa mara ya kwanza.
Baada ya kuuza Beats, alinunua jumba kubwa la kifahari Los Angeles la ukubwa wa futi 14,000 mraba kwa $40m (£31m).
Rapa ambaye pia ni mmiliki mwenza wa Cash Money Records Bryan "Birdman" Williams ana utajiri wa $110m (£85m).
Drake utajiri wake unakadiriwa kuwa $90m (£70m).
Pamoja na kulipwa kutokana an mauzo ya muziki wake, pia ana mikataba ya kibiashara na Apple, Nike na Sprite.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni