Rais mpya wa shirikisho la kandanda barani Afrika (CAF) Ahmad, amesema amekataa mshahara kutoka kwa shrikisho hilo.
Kuchaguliwa kwake mwezi Machi kulimaliza uongozi wa raia wa Cameroon Issa Hayatou wa miaka 29."Nimekataa mshahara wa (CAF) kwa sababu iliyo rahisi, CAF haieshimu uongozi mzuri," aliiambia BBC.
Mishahara ya wafanyakazi wa CAF, kuanzia wasimamizi na kamati wakurugenzi hadi Rais inastahili kuwa na uwasi.
Anataka pia kushughulikia suala la uwekezaji wa CAF kusaidia kuboresha mchezo wa kandanda kote barani, akisema kuwa wajibu wa CAF sio kutengeneza pesa na kujitajirisha.
Source:BBCSwahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni