Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameteua baraza la mawaziri lenye usawa wa kijinsia kuambatana na ahadi ya mapema ambapo 11 kati ya mawaziri 22 ni wanawake.
Sylvie Goulard ndiye waziri mpya wa ulinzi huku bingwa wa olimpiki wa mchezo wa kupigana na panga Laura Flesseng, akiteuliwa kuwa waziri wa michezo.
Bruno Le Maire ameteuliwa kuwa waziri wa uchumi, Gérard Collomb waziri wa masuala ya ndani, huku naye François Bayrou ndiye waziri wa sheria.
Rais huyo mpya wa Ufaransa ana matumaini kuwa kikosi hicho kitazoa kura nyingi kwenye uchaguzi wa ubunge mwezi ujao.
- Macron ashinda uchaguzi wa urais Ufaransa
- Macron ataka marekebisho makubwa Ulaya
- Macron amchagua meya kuwa waziri mkuu Ufaransa
Alitimiza ahadi yake ya kuwepo usawa kwenye baraza la mawaziri, lakini kati ya nafasi muhimu tano , ni moja ya tu ya ulinzi ilimuendea mwanamke.
Mawaziri wengine ni pamoja na Jean-Yves Le Driana, ambaye ameteuiliwa kuwa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni.
Wengine ni pamoja na:
- Agnès Buzyn - Afya
- Murielle Pénicaud - Kazi
- Mounir Mahjoubi - Masuala ya dijitali
- Françoise Nyssen - Utamaduni
- Jean-Michel Blanquer - Elimu ya taiafa
- Jacques Mézard - Kilimo na chakula
- Source:BBCSwahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni