Rais wa Afrika
Kusini Jacob Zuma anatarajiwa kuzuru nchini Tanzania hii leo katika
ziara ya rasmi ya siku tatu kufuatia mwaliko wa rais John Pombe
Magufuli.
Akizungumza na vyombo vya habari siku ya Jumatatu Waziri
wa maswala ya kigeni nchini Tanzania Augustine Mahiga alisema kuwa
ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara mbali kuangazia
maswala mbali mbali ya maendeleo.Rais Zuma ataandamana na mawaziri sita pamoja na wafanyibiashara kadhaa kutoka Afrika Kusini.
- Zuma adaiwa kusinzia bungeni
- Waandamanaji wanakusanyika kumpinga Zuma
- Jacob Zuma : Siogopi kufungwa jela
- Rais wa zamani Afrika Kusini ampinga Jacob Zuma
Kulingana na Mahiga kiwango cha biashara kati ya mataifa hayo mawili kimeongezeka kutoka dola milioni 803 mwaka 2006 hadi dola bilioni 2.2 2016 hatua iliobuni ajira 20,916.
Source:BBCSwahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni