Mwanamke mmoja nchini Colombia
alitafuna na kumeza pesa zote alizokuwa amejiwekea kama akiba, kuzuia
mumewe asizichukue na kuzitumia.
Sandra Milena Almeida alimeza £7,000 ($9,000) baada ya kugundua kwamba mumewe alikuwa na mpenzi mwingine.Hatua yake iligunduliwa baada yake kukimbizwa hospitalini akilalamika kutokana na maumivu makali tumboni.
Madaktari walipata mabunda ya noti katika tumbo lake.
Bi Almeida, 30, yamkini awali alificha pesa hizo baada ya kusikia taarifa kwamba mumewe hakuwa mwaminifu kwake.
Lakini aliamua kuzila noti hizo za $100 baada ya mumewe kugundua eneo alimokuwa ameficha pesa hizo na kudai agawiwe nusu yake.
Jamaa na madaktari waligundua kitendo alichokuwa amefanya mwanamke huyo baada ya kumpima.
![]() |
| Noti zilizotolewa tumboni mwa Sandra |
"Nyingine zilipatikana katika utumbo wake mkubwa."
"Yamkini kilikuwa kitendo cha kutamauka, kutokana na tatizo lililomkabili. Hili bila shaka lilimwathiri tumbo."
Mrs Almeida, anayetoka Piedecuesta, anatarajiwa kupata nafuu kabisa baada ya upasuaji huo.
![]() |
| Bw Serranoa anasema mwanzoni alidhani mwanamke huyo alikuwa mlanguzi wa mihadarati |
Hata hivyo kunazo ambazo ziliathiriwa na kemikali tumboni.
Bi Almeida amesema sasa ataweka akiba pesa za kwenda likizo ya kifahari
Source:BBCSwahili



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni