YoungConciousâ„¢

Be Updated on the World of Sports, latest News and Entertainment Stories.

Propellerads

Breaking News

Translate

Welcome to Young concious .blogspot.com ==>>Feel free to leave your comment

Jumatatu, 15 Mei 2017

Milio ya risasi yatanda miji mikuu Ivory Coast



Wanajeshi waasi mjini Bouake, Mei 14, 2017Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWanajeshi hao waasi walimsaidia Ouattara kuchukua uongozi 2011
Ufyatulianaji mkali wa risasi umezuka katika miji miwili mikuu nchini Ivory Coast, wanajeshi wakiendelea kuasi kwa siku ya nne mtawalia.
Wanajeshi hao waliogoma wamefunga barabara nje ya kambi za jeshi katika mtaa wa kifahari Abidjan, mji mkuu wa kibiashara wa Ivory Coast, mwandishi wa BBC mjini humo anasema.
Wanajeshi watiifu kwa serikali wameelekea katika mji wa pili, Bouaké, ambapo ufyatulianaji wa risasi pia umesikika.
Mkuu wa majeshi ya nchi hiyo Jenerali Sékou Touré ameapa kumaliza maasi hayo, ambayo yalitokana na mzozo kuhusu malipo.
Kupitia taarifa Jumapili, Jenerali Touré alisema wengi wa wamnajeshi hao waliogoma walikuwa awali wameitikia wito wa kuwataka wasitishe mgomo wao.
Lakini operesheni ya kijeshi imeanzishwa kwa sababu baadhi ya wanajeshi wameendelea kupuuza maagizo ya wakuu wao, amesema.
Wanajeshi hao waasi wameapa kujibu mashambulio iwapo watakabiliwa na wanajeshi watiifu kwa serikali.
Milio ya risasi imesikika katika kambi ya jeshi ya Akouédo, mtaa ambao huwa na wakazi wengi wa mapato ya wastani nchini Ivory Coast na ambapo pia raia wa kigeni hupenda sana kuishi, mwandishi wa BBC aliyepo Abidjan Tamasin Ford anasema.
Mwanajeshi aliyegoma Bouake, Mei 14, 2017
Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWanajeshi waliogoma wanadhibiti mji wa Bouaké, mji wa pili kwa ukubwa Ivory Coast
Serikali imepungukiwa na pesa kutokana na kushuka kwa bei ya zao la kakao, jambo linaloifanya vigumu kwa serikali kutimiza madai ya wanajeshi hao.
Mzozo huo wa sasa umezua wasiwasi wa kuzuka tena kwa ghasia zilizoshuhudiwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka kumi nchini Ivory Coast, ambavyo vilimalizika mwaka 2011.
Wengi wa wanajeshi hao waasi, ambao walianza kuasi Januari, ni waasi wa zamani ambao walijiunga na jeshi baada ya kumalizika kwa vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe.
Walimsaidia Rais Alassane Ouattara kuchukua uongozi 2010 baada ya mtangulizi wake Laurent Gbagbo kukataa kushindwa katika uchaguzi mkuu.
map
Walianza kuasi mara ya kwanza Januari na kuilazimisha serikali kuahidi kuwalipa jumla ya $8,000 (£6,200) kila mmoja kama sehemu ya malimbikizi ya marupurupu.
Walitarajiwa kupokea malipo zaidi mwezi huu na baadhi ya wanajeshi walikasirika kwamba msemaji wao Alhamisi alisema watatupilia mbali madai yao ya kutaka kulipwa pesa zilizosalia.
Serikali imesema haitafanya mazungumzo na wanajeshi hao.
Ivory Coast ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi wa kakao duniani, na zao hilo hutegemewa sana na taifa hilo kujipatia fedha za kigeni

Source:BBCSwahili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Propellerads