Shirikisho la soka
duniani FIFA chini ya raisi wake mpya Gianni Infantino linaonekana
kujaribu kuinua sana soka katika ukanda wa Afrika, ambako kuna wafuasi
wengi wa Infantino.
Shirikisho hilo la soka sasa limeamua kuipa
Africa nafasi ya upendeleo kwa kuiongezea nafasi 5 zaidi za ushiriki
katika fainali za kombe la dunia la mwaka 2026.Katika fainali hizo timu
zitaongezeka kutoka 36 hadi 48 na Afrika itawakilishwa na timu 9 ambapo
nyingine ya 10 itapambana katika hatua ya mtoano.Shirikisho hilo pia limeongeza idadi ya timu kutoka katika bara la Ulaya ambapo mwanzoni zilikuwa ni timu 13 na sasa zitakuwa 16, huku Marekani Kaskazini na kusini zikiwa timu 6 badala ya 3.
Oceania nao wamepewa nafasi moja ya uwakilishi wa moja kwa moja ambapo hapo mwanzo iliwapasa wacheze mchezo wa mtoano na timu za Amerika Kusini ili kufudhu.
Hii itawafanya New Zealand kuwa na nafasi kubwa ya kushiriki kombe la dunia kila mara kutoka na kutokuwa na upinzani mkubwa haswa baada ya Australia kuanza kushiriki michuano ya bara la Asia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni