Jumla ya visa 18
vya ugonjwa wa Ebola vimeripotiwa nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo
kwa mujibu wa shirika la afya Duniani WHO.
Vifo vya watu watatu vimeripotiwa kutokana na ugonjwa huo.Waliokufa ni pamoja na mwanamume wa umri wa miaka 39 aliyetajwa kuwa "mgonjwa sufuri" na watu wawili ambao walikuwa wamekaribiana naye, WHO ilisema.
WHO iliongeza kuwa takwimu zake zinaonyesha kuwa kuna hatari kubwa eneo hilo na ndogo katika maeneo ya kimataifa
WHO ilitangaza mlipuko wa ugonjwa huo nchini DRC wiki iliyopita.
Zaidi ya watu 11,000 walifariki kutokana na ugonjwa wa Ebola magharibi mwa Afrika mwaka 2014 na 2015 hasa nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia.
Source:BBCSwahili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni